Olivier Giroud alifunga bao la pili kwake na la nne kwa Arsenal (HM)
Lukas Podolski naye alifunga bao
Wachezaji wa Arsenal wakishangilia ushindi
MSHAMBULIAJI Olivier Giroud amefanya kazi nzuri ya kumshawishi kocha Arsene Wenger kwamba hahitaji kusajili mshambuliaji mpya majira haya ya joto kwa kufunga mabao mawili katika ushindi wa 7-0 dhidi ya Indonesia XI kwenye Uwanja wa Gelora Bung Karno, katika mchezo wa kwanza wa Arsenal kwenye ziara ya kujiandaa na msimu.
Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ufaransa, ambaye alikuwa mshambuliaji chaguo la kwanza wa kati wa The Gunners msimu uliopita, alifunga mabao mawili ndani ya dakika nne mjini Jakarta baada ya kuingia akitokea benchi na kumkumbusha Wenger kwamba yeye anaweza kazi.
Arsene Wenger alianzisha kikosi cha nguvu katika mchezo huo wa kwanza wa kujiandaa na msimu, akiwapanga nyota kama Mikel Arteta, Per Mertesacker, Theo Walcott, Alex Oxlade-Chamberlain, Aaron Ramsey na Kieran Gibbs.
Mabao mengine ya Arsenal yalifungwa na Walcott dakika ya 19, Akpom dakika ya 54, Podolski dakika ya 83, Olsson dakika ya 85 na Eisfeld dakika ya 87.
Kikosi cha Arsenal kilikuwa; Fabianski/Martinez dk68, Jenkinson/Sagna dk68, Miquel, Mertesacker/Koscielny dk46, Gibbs; Arteta/Zelalem dk46, Ramsey/Rosicky dk68, Oxlade-Chamberlain/Olsson dk46; Gnabry/Podolski dk68, Akpom/Giroud dk68, Walcott/Eisfeld dk46.
Chanzo: binzubeiry
No comments: