» »Unlabelled » COMING SOON > EDA … KUKOSA MTOTO NA USHAWISHI WA KUTOKA NJE YA NDOA …






EDA  ni kipindi kisichopungua miezi mitatu ambacho anapaswa kukaa mwanamke bila kuolewa wala kushirikiana na mwanamume ama baada ya kutengana na mumewe au baada ya kufiwa na mume.Hii ni kwa mujibu wa dini ya kiislam.
EDA ni filam inayochambua changamoto za maisha ya ndoa katika familia nyingi.

Ndani ya filamu hii yumo Ussi Hajji  kama YUSSUF. Marry Mwita kama YUSRA.Hidaya Njaidi na Abrahman Thomas kama wazazi wa Yusuf.Hashim Kambi na Khadija Ibrahim kama wazazi wa Yusra. Gerry wa Rymes kama OMAR rafiki wa YUSSUF, Sabrina Rupia kama KHAYRA mtumishi wa kampuni ya YUSSUF na rafiki wa yusra. Ahmed Olotu kama mwalimu wa dini. n.k
YUSSUF  ni mtu mwenye uwezo  mzuri kimaisha na wanaishi maisha ya furaha na  uchamungu na mkewe YUSRA.YUSSUF yuko busy sana na masuala ya kazi, wanachelewa kupata mtoto jambo linalopelekea wazazi wa YUSSUF kumsakama  mtoto wao wakitaka amwache mkewe wakidhani ndiye mwenye tatizo. 
Huku wazazi wa YUSRA wakimsakama mtoto wao wakitaka atafute suluhisho mapema kabla tatizo hilo halijazua mtafaruku. YUSSUF na YUSRA wanakuwa katika hali ya mashaka ingawa wataalamu wa afya wamewathibitishia kuwa hakuna mwenye tatizo kati yao.
  Jambo hili linawafanya wawashirikishe hata marafiki kwa nyakati tofauti. Hatimaye YUSRA anatafuta ushauri  kwa KHAYRA ili kunusuru ndoa yake.
KHAYRA anamtumbukiza katika njia ngumu. YUSRA anaomba pesa toka kwa mumewe afanye biashara. YUSSUF anampa milioni tano.YUSRA anchukua pesa hizo na kumpelekea OMAR, rafiki wa mumewe. Anamwomba awe naye ili apate ujauzito kama alivyoshauriwa na KHAYRA, anusuru ndoa yake.
Lakini OMAR anamwogopa MUNGU na kuthamini utu wake. Anakataa na kumrudishia taarifa hizo YUSSUF akimwomba amkanye mkewe.
 YUSSUF anakasirika na kumpa talaka moja mkewe. Wazazi wanachanganyikiwa . mama yake YUSRA anamlaumu mwanawe kwa kuchukua ushauri toka kwa rafiki  asiye na ushauri mwema. 
YUSRA anaingia katika EDA ya talaka…. Kwa mujibu wa sheria ya kiislam.
Poster-24x36 (1)2 
Siku 7 kabla ya EDA kwisha. Mama YUSRA anampigia simu YUSSUF kuwa mkewe yu mjamzito. YUSSUF anafurahi sana.  Ananuwia kumrejea mkewe.
Akiwa njiani kwenda kumrejea mkewe anapata ajali na kukutwa na mauti. Jambo linalomfanya YUSRA kuingia katika EDA nyingine ya kufiwa na mume kwa mujibu wa sheria ya kiislam.
HII NI BONGE LA FILAMU KUTOKA TANZANIA NA IKO NJIANI, ITATOKA TAREHE 27 MWEZI HUU … YAANI JUMATATU … KAA MKAO WA KULA.

Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply