Kitu kizuri kuhusu kushiriki Big Brother Africa ni kwamba hata kama usiposhinda, tayari utakuwa staa kwenye nchi yako. Jana mwakilishi wa Zimbabwe kwenye Big Brother Africa (BBA): The Chase Pokello Nare aka The ‘Queen of swagger’ alipokelewa na umati mkubwa jijini Harare.
Mashabiki walipelekwa na usafiri wa bure hadi kwenye uwanja wa ndege wa Harare na mabasi matatu, luxury coaches na malori wakiwa wamevaa kofia zenye jina la Pokello.
Aliyekuwa mshiriki mwenzake Hakeem Mandaza, maafisa wa mamlaka ya Utalii nchini (ZTA) na wengine walikuwa miongoni mwa watu waliojitokeza kumpokea.
No comments: