Mwigizaji aliyeibua vipaji vingi sana hapa nchini Lucy Komba, ameigiza Filamu yake mpya na mume wa mwigizaji mwenzake Irene Uwoya Hamad Ndikumana maarufu kama Katauti.
Katika habari iliyopo kwenye ukurasa wake wa facebook mwanadada huyo ametoa picha ya cover la Filamu hiyo yake mpya iliyopewa jina la “Kwanini nisimuoe”
Filama hiyo ambayo imetengenezwa kutokana na kisa cha kweli inatarajiwa kutoka hivi karibuni.
Akiizungumzia Filamu hiyo Lucy amesema kuwa itakuwa ya tofauti kidogo kwani kipaji cha Hamad katauti ni ca aina yake.
No comments: