» » » » Mtangazaji wa EATV kwenye kipindi cha Wanawake Live Joyce Kiria Afiwa na Baba yake Mzazi, Kusafirisha Leo



Mtangazaji wa kipindi cha ‘WANAWAKE LIVE’ kinachorushwa kupitia EATV Joyce Kiria amefiwa na baba yake mzazi aitwaye Michael Francis Lwambo jana Jumatano (July 10) aliyekuwa akiishi mkoani Tanga.
Joyce Kiria
Taarifa iliyotolewa na Kiria jana (July 10) kupitia kupitia website yake joycekiria.com inasema mwili wa marehemu utasafirishwa leo alhamisi (July 11) kuelekea Moshi kwa ajili ya taratibu za mazishi.
Joyce aliandika:
“Leo ni siku nyingine ya Historia kwenye maisha yangu baada ya baba yangu Michael Francis Iwambo Kiria wa kibosho dakau nganyeni kufariki huko mkoani Tanga ambako alikuwa akiishi. Kesho ni safari ya kuelekea moshi kwa ajili ya taratibu za mazishi.
Im speechless…… RIP MY DADY”
Bongo 61 Team Tunampa pole Joyce Kiria kwa msiba uliomkuta, na Mungu ailaze mahala pema roho ya marehemu Michael Francis Iwambo, Amen

Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply