Ni habari za kusikitisha,Mama mzazi wa Profesa Jay ‘Mama Majanjala amefariki dunia baada ya jana usiku kugongwa na gari wakati akivuka barabara maeneo ya Mbezi jijini Dar es Salaam.
Profesa Jay akiwa na marehemu mama yake (aliyemshika begani)
Mdogo wake na Profesa Jay, Black Rhyno amesema alipokea taarifa za kifo cha mama yake usiku baada ya kuwa ametoka kazini ambapo awali alipigiwa simu na baba yake mzazi ambayo hata hivyo hakuweza kuipokea na baadaye kaka yake Jay alimpigia kumpa taarifa hizo.
“Yaani nilikuwa sijui chochote,” amesema Black Rhyno.”
Black Rhyno
“Akaniambia amepata ajali, Mbezi huko kwasababu Jay alikuwa anakaa naye, amegongwa na gari, hapa kituo cha Mbezi, Mbezi mwisho, hiki kituo kipya, kuna gari moja ndogo, Starlet mtu alikuwa anaandesha, nadhani mama yeye alikuwa anavuka barabara kwa upande wa pili kwenda kununua kitu kwahiyo huyo mtu akawa amemgonga.”
Black amesema baada ya mtu huyo kumgonga mama yao, alimchukua wakaenda hospitali kuchukua PF3 kabla ya kumkimbiza hadi katika hospitali ya Tumbi kwa Bajaj.
“Wakati wameenda polisi mama alikuwa vizuri tu, ametoa maelezo yake yote vizuri, ameandika jina lake, ameeleza kila kitu, akapiga simu kwa Jay akamwambia ‘mimi nimepata ajali’, akawaambia askari ‘ongeeni na mwanangu huyu hapa Profesa Jay.”
“Wakati (Profesa) hajaambiwa kwamba mama amefariki wakati wao (mama yake na dereva aliyemgonga) wakitoka hapa kituo cha Mbezi Luis kwenda Tumbi, Jay alikuwa anamtafuta kwenye simu baadaye akamfuata na alikuwa ameshafikishwa hospitali. Alivyompata (kwenye simu) akawa anaongea naye akawa anamuambia ‘mwanangu nimegongwa najisikia vibaya, mwanangu nakufa nakufa’.
Alimpigia simu kila mtu lakini Jay mwishoni alikuja kumpata alimwambia kwamba ‘nakufa mwanangu’. Jay alikuwa anasema’mimi nilikuwa nachukulia tu kwamba mama atakuwa tu na uoga’. Baadaye kwenye simu akawa haongei tena, akamwita mama mtu mwingine akapokea simu, akawambia ni nesi wa hapo Tumbi, ndo akapokea akamwambia kwamba tupo na Mama hapa tunamhudimia, akamwambia ‘naomba niongee naye’ ‘hatuwezi kumpa sababu tumeanza kumwekea PoP kwenye mguu’,sababu alikuwa analalamika maumivu kwenye kichwa na kwenye mguu. Lakini Jay anasema muda ule wakati anamwambia ‘nakufa nakufa’ ndio alikuwa mtu wa mwisho anaongea na akakata roho.”
Black Rhyno amesema bado wanasubiri report ya daktari ili kujua sababu ya kifo cha mama yao.
“Bado mwili upo Tumbi na mpaka sasa tunasubiri uchunguzi huo wa post-mortem,”amesema. Ameeleza kuwa msiba upo nyumbani kwa Profesa Jay, Mbezi Dar es Salaam.
Mungu ailaze roho ya Mama Majanjala mahali pema peponi na tunawapa pole Profesa Jay na Black Rhyno kwa kufiwa na mama yao.
Msikilize zaidi Black Rhyno hapa.
No comments: