» » » Soma ripoti mpya ya Wizara ya elimu kuhusu waliochaguliwa kidato cha 5 2013?



Wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi imesema Wanafunzi elfu 34,213 ndio wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano kwenye shule za sekondari za Serikali pamoja na vyuo vya ufundi mwaka 2013 ikiwa ni ongezeko la Wanafunzi 2,790 sawa na asilimia 8.9 ikilinganishwa na Wanafunzi elfu 31,423 waliochaguliwa mwaka 2012.
Naibu Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Philipho Mulugo amesema nafasi zilizopo kwa Wanafunzi wa kidato cha tano mwaka huu ni 43,757 zikiwemo za masomo ya Sayansi 18,564 na masomo ya Sayansi ya jamii 25,193 ikiwa ni ongezeko la nafasi 3,757 ikilinganishwa na nafasi 41,000 zilizokuwepo mwaka jana.
Naibu Waziri anakwambia Wanafunzi waliochaguliwa wamepangiwa kwenye shule 207 Tanzania na kutokana na uchache wa Wanafunzi wenye sifa za kujiunga na kidato cha tano hasa kwa masomo ya Sayansi ya jamii, Serikali haikuweza kuongeza zaidi shule mpya za kidato cha tano mwaka huu.
‘Kwa kidato cha tano peke yake kama form V ni Wanafunzi 33 mia sita 83 na Ufundi peke yake ni mia tano thelathini, hilo ni ongezeko la Wanafunzi 2790, Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano peke yao  elfu 33 na 683 wakiwemo Wavulana elfu 23, 383 na Wasichana elfu 10,300 ndio wamechaguliwa kujiunga na form V kwenye shule za Serikali mwaka huu ambapo hiyo idadi ni ongezeko la Wanafunzi elfu mbili mia nane na ishirini na nne sawa na asilimia 9.15′ – Mulugo
.
Mbabala Sekondari, moja ya shule ambazo Wanafunzi wamekiri wanasomea pagumu
Kwenye sentensi nyingine Mulugo ametiririka kwa kusema asilimia 58.62 ya Wanafunzi wamechaguliwa kusoma masomo ya Sayansi na asilimi 41.38 wamechaguliwa kusoma masomo ya Sayansi ya jamii huku Wanafunzi 76 waliokua na sifa za msingi hawajachaguliwa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kuzidi umri wa miaka 25.
Namkariri Mulugo akisema “Serikali ina umri wa Wanafunzi kuanza ngazi fulani kwenda ngazi fulani kwahiyo wengine tumekuta wana umri wa miaka 28 wengine 32 na 35 pia mwingine hakua raia wa Tanzania, wengine wamekosa combination yani unafaulu lakini unakosa combination’
Wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano wanatakiwa kuripoti kwenye shule walizopangiwa July 29 2013.

Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply