» » » Video queen Vera Sidika wa Kenya apata dili ya kuwa ‘cover model’ wa jarida la ‘King Magazine’ la Marekani



Tunapomzungumzia Vera Sidika aka Vee S. beiby au kama wakenya wanavyopenda kumuita ‘miss Big booty’ nakuwa namaanisha yule mrembo aliyeipamba video ya P. Unit ‘You Guy’. Uzuri wa mrembo huyo umemfanya aweze kuteka hisia za mashabiki wengi (hususan wanaume) lakini pia unamsaidia kupata michongo mbalimbali hata nje ya nchi yake.
vera 22
Mtandao wa Daily Post wa Kenya umeripoti kuwa Vera amepata dili ya kutokea katika jarida la wanaume ‘King Magazine’ la Marekani kama ‘cover model’ katika toleo lijalo. King Magazine ni jarida la ‘African-American’ kwaajili ya wanaume ambalo huandika habari za watu maarufu, hip hop, fashion, michezo pamoja na warembo wa videos ‘video vexens’.
vera-2
Shavu hili limekuja ikiwa ni siku chache tu toka Vera atokee katika top ten ya video vixens wa Africa iliyotolewa na Channel O akikamata nafasi ya 4.

Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply