Mshambualiaji wa Man United, Wayne Rooney (HM)
Kocha wa Man United, David Moyes
WAZI Wayne Rooney anaonekana anataka kuondoka Manchester United kabla ya mwanzo wa msimu mpya baada ya kukerwa na jinsi anavyochukuliwa juu ya mustakabali wake katika klabu hiyo.
Chelsea na Arsenal zote zinamtaka mshambuliaji huyo England, ambaye ameripotiwa kukasirika na kuchanganyikiwa na jinsi anavyofanyiwa na maneno ya kocha mpya wa United, David Moyes.
Moyes amesema Rooney ni muhimu kikosini - iwapo Robin van Persie anakuwa majeruhi.
Hii imechukuliwa kwamba Moyes anamshusha Rooney mbele ya Mholanzi huyo mkali wa mabao.
Na akiwa ameweka nyumbani Medali za mataji manne ya Ligi Kuu England na moja la Ligi ya Mabingwa kwa jina lake, Rooney haamini kama ana chochote cha zaida cha kuthibitisha United.
Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho alizungumzia nia yake kwa Rooney, akisema: "Ni mchezaji ninayempenda sana, lakini siwezi kusema zaidi. Ana kasi na anayepasua na ninampenda. Lakini ni mchezaji wa Manchester United player,".
Jumanne alikuwa radhi kumzungumzia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alipoiambia BBC Sport: "Ikiwa Wayne ni chaguo la pili kwa Man United, kisha timu ya taifa itaathirika,".
"Hiki ni kipindi ambacho klabu kubwa na makocha wao wanahusishwa na kila kitu,"alisema Mourinho. "Hadi Agosti 31, huo ndiyo utakuwa mwisho wa tetesi na ukweli utabainika,".
Akiwa anatakiwa na klabu za Chelsea na Arsenal pamoja na PSG, tayari United imetoa msimamo wake, ikisema haitamuuza mchezzji huyo kwa klabu yoyote pinzani kwao.
Chanzo: binzubeiry
No comments: