» » ANDER HERRERA YUPO RADHI KUHAMIA MAN UNITED MWEZI JANUARY


herrera_deafa.jpg

Ander Herrera ameonyesha wazi kwamba yupo tayari kujiunga na Manchester United mnamo mwezi January.
Kiungo huyo wa Athletic Bilbao alikuwa akitakiwa na United na ikatumwa ofa ya £26m kwa ajili ya kumnunua na ikapigwa chini na Bilbao - huku wakisisitiza mchezaji atauzwa mara tu United watakapolipa kiasi cha £30.5m ili kuvunja mkataba wao na mchezaji huyo.(P.T)
Herrera, 24, alisema: 'Ilikuja ofa kutoka kwa United na naweza kuona hilo ni jambo zuri kwa maana wamevutiwa na kiwango changu.
'Pamoja na kuripotiwa nilifanya vipimo vya afya au kukubaliana na United, lakini chochote kilichotokea baina yangu na klabu hiyo. Ukiniuliza kuhusu usajili huko mbeleni, lolote linaweza kutokea.'
Herrera pia amewakana kabisa wanasheria watatu ambao walifika kwenye ofisi za La Liga kwenda kufanya mazungumo juu ya kipengele cha kuvunja mkataba wa mchezaji huyo na Bilbao.
Chanzo:Shaffih Dauda

'Sina uhasiano wowote na wale watu watatu ambao walienda kwenye ofisi za ligi - na naweza kusema hawakuwa na lolote kwa pamoja na wawilikilishi wangu.'

Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply