Miss Universe 2012, Olivia Culpo yupo matatani na kama akipatikana na hatia anaweza kwenda jela miaka miwili kwa kuvunja sheria kwenye eneo la kihistoria linaloheshimika sana nchini India, Taj Mahal.
Mrembo huyo alikuwa akipiga picha za tangazo la sandals.
Kwa mujibu wa sheria za India, ni marufuku kufanya shughuli zote za kufanya tangazo kwenye eneo hilo. Miss Universe yupo kwenye ziara ya siku 10 kuhamasisha masuala ya utetezi wa wanawake na uelewa kuhusu Ukimwi nchini humo.
No comments: