» » Watumiaji wa Facebook Hii Inawahusu



Mtandao maarufu wa kijamii Duniani wa Facebook umeondoa option iliyokuwa ikitumiwa na watu wengi wanaopenda kuwa na privacy au wasiopenda baadhi ya watu wasiwapate kwa kusearch majina yao kwenye timeline.



Sasa hivi kama unajua kuna mtu hutaki akuone upo facebook au asione unachokipost katika mtandao huo basi una option mbili tu, kujiondoa kabisa facebook, au kuacha akuone sababu huwezi tena kwenda katika option ya ‘Who can look up your timeline by name?’ sababu haipo.

Mtandao huo tayari umeiondoa huduma hiyo kwa watumiaji ambao walikuwa hawajaitumia option hiyo mwaka jana, na kwa wale ambao walikuwa wame activate huduma hiyo, muda wowote kuanzia sasa hawataiona tena.

Kabla ya mabadiliko hayo ilikuwa inawezekana kwa mtumiaji mwenye akaunti facebook kuhide profile zao ili mtu ambaye si rafiki asiweze kumpata kwa kusearch jina lake katika search box huku mtumiaji huyo yupo facebook

Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply