Only God can judge me, is that right? (Only God can judge me now) Only God baby, nobody else, nobody else, all you other motherfu***rs get out my business,” ni mashairi ya wimbo wa Tupac yaliyomuingia Lulu hadi kuamua kujichora tattoo yenye maneno hayo, Only God can judge me – Ni Mungu pekee anayeweza kunihukumu.
Kupitia Instagram, muigizaji huyo wa Foolish Age, ameonesha picha ya tattoo hiyo na kuwapa ujumbe wale wanaofuatilia maisha yake.
“Kumekuwa na kawaida ya watu kuongea na kuhukumu wenzao bila ya kujua wanachokiongelea pengine!!Kwa upeo Wangu mdogo nafahamu sisi wote ni binadamu na tunamtegemea mtu mmoja MWENYEZI MUNGU…lakini cha kushangaza Kuwa watu wako busy kuhukumu wenzao kuliko hata huyo mwenye cheo chake…Hivi Mungu angetaka kufanya Kama wanadamu tunavyofanya tungeangaliana kweli….Nadhani umefika wakati wa kumuachia mwenye majukumu yake kufanya kazi…tuache kujipa u busy usio wa lazma….!!!ONLY GOD CAN JUDGE ME,” ameandika.
No comments: