Pamoja na ziara ya Ommy Dimpoz nchini Marekani kumuingizia mpunga, inazidi kumtengenezea connections zaidi.
Ommy Dimpoz akiwa na Tuface
Staa wa muziki nchini Nigeria, Tuface Idibia weekend hii alikutana na Ommy Dimpoz huko Hollywood, jijini Los Angeles, Marekani na kukubali mwaliko wa kuhudhuria show ya hitmaker huyo wa Tupogo.
Ommy Dimpoz akisalimiana na Tuface
“Kakubali sana kazi zangu, hasa Me and You na Tupogo, so sasa hivi siwezi kuweka wazi mpaka mambo yakae sawa,” Ommy ameiambia Bongo5 kuhusiana na kama kuna uwezekano wa wawili hao kufanya wimbo pamoja.
Ommy Dimpoz na Tuface wakibadilishana mawili matatu
Katika hatua nyingine, Ommy amesema amekuwa msanii wa kwanza Tanzania kufanya show Hollywood.
No comments: