Mtoto wa tajiri namba moja nchini, Said Bakhresa, aitwaye Yusuf amenunua na kuileta nchini gari ya thamani aina ya Brabus B63-620.
Gari ya Yusuf Bakhresa
Gari hilo limetengenezwa kwa oda maalum na ndani limeandikwa jina la Yusuf ambapo ndani limeandikwa ‘Special Edition for Yusuf Bakhresa’.Brabus ni kampuni inayotengeneza kwa kucustomize magari ya Mercedes-Benz, Smart na Maybach.
Gharama ya gari hilo ni takriban dola 500,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 800 za Tanzania.
Wateja wa magari ya Barbus wanaweza kununua moja kwa moja kutoka Brabus ama kutuma gari zao za Mercedes kuwa customized. Kama mteja akiagiza gari kutoka Brabus, Brabus hununua gari kutoka Mercedes na kuiboresha kwa matakwa ya mteja. Brabus inajulikana kwa kucustomise magari ya thamani kubwa na kuzifanya ziwe na mtazamo wa, “if you have to ask the price, you can’t afford it”
Ukiongeza na gharama za special edition na za kuileta nchini, gari hiyo inaweza kuwa imemgharimu zaidi ya shilingi bilioni 1.
Dereva wa gari hilo
Brabus, ni kampuni ya Ujerumani iliyoanzishwa mwaka 1977 na Prof. Bodo BUSchmann na Klaus BRAckman.
Image Credit: Bin Zubeiry
No comments: