Kumekua na tetesi zilizoenea katika mitandao siku mbili hizi pamoja na picha zinazowaonesha Naseeb Abdul aka Diamond Platnumz akiwa katika pozi la ‘more than a friend’ na mpenzi wake wa zamani ‘drama queen’ CEO wa Endless Fame Wema Abraham Sepetu. Habari hizo zilidai kuwa kuna mapenzi ambayo bado yana exist kati ya wawili hao.
Wema Sepetu na Diamond
Hii ndio picha aliyopost Diamond mwenyewe jana Instagram jana
Baada ya taarifa hizo kuzagaa mpaka katika magazeti ya udaku juzi (October 8) Diamond alikana kupitia blog yake ya This is diamond kwa kusema “I REAL LOVE MY PENNY,SIJARUDIANA NA WEMA”.
Katika hatua nyingine jana (October 9) kupitia Instagram rais huyo wa wasafi amepost picha akiwa na Wema sehemu inayoonekana kuwa ni nje ya Tanzania wakiwa katika pozi la ukaribu wa zaidi ya urafiki, kisha picha hiyo imesindikizwa na caption,
“Katika moja ya Muvie ambazo naimani itakuwa ni Gumzo, Mfano na Bora toka Tanzania basi ni hii… #TEMPTATIONS …. STAY TUNED!!!! SOON!….#DayOne #Location #SomeWhere”aliandika Platnumz
Na hizi (chini) ni kati ya picha za Wema na Diamond zilizosambaa mtandaoni hivi karibuni
Well, je hii inamaanisha hata picha hizi zilizosambaa awali zinahusiana na movie hiyo? Yote tisa, kumi kama kweli kuna movie inakuja kati ya wawili hao naamini itakuwa one of the best movies in Tanzania kutokana na historia yao hususani ya mapenzi na ina kila dalili ya kufanya vizuri sokoni kutokana pia na majina yao makubwa. Fursa!
No comments: