» » » Poppin: Baba Levo atangaza kubadili jina lake na kuacha kufanya hip hop (Audio)


Msanii wa Kigoma Allstars, Clayton Revocatus aka Baba Levo ametangaza kubadilisha jina lake ambapo kuanzia sasa anataka ajulikane kama ‘Baba la Baba’.
baba-levo
Baba Levo (kushoto) akiwa na Zitto Kabwe
Akiongea na kituo cha radio cha Bomba FM cha Mbeya kwenye kipindi cha Kali za Bomba, msanii huyo wa TMK amesema ataachia wimbo wake mpya uitwao Baba la Baba ili kulitambulisha jina lake jipya. Alisema sababu ya kujiita Baba la Baba ni kutokana na baba yake na pia mwanae wote kuitwa Revocatus.
“Kwahiyo mimi nimemzaa baba yangu kupitia jina, kwahiyo mimi ni baba yake na baba, kwahiyo mimi ni baba la baba,” alisema. Katika katua nyingine, msanii huyo amesema ameachana na hip hop baada ya kuona mazingira ya hip hop kwake yanakuwa magumu kuweza kupata hela.
“Kuna watu wanafanya hip hop na wanapata hela lakini upande wangu mimi nikaona inakuwa ni ngumu, inaniwekea mazingira magumu sana kuweza kupata pesa. Nikajaribu kupigia muziki wa kidunia kwaajili ya kuchezea raia nikaona kidogo Mungu anasaidia riziki inapatikana. Kwahiyo ikabidi nikomae huko huko na nimeweza kuimaster hiyo style.”


Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply