Kwa mujibu wa BBC, mke wa zamani wa Mandela, Winnie Madikizela-Mandela amesema kuwa rais huyo wa zamani hawezi kuzungumza, lakini anatumia uso kuwasiliana na watu.
Ameongeza kuwa jumla ya madaktari 22 wanaendelea kumpa huduma ya matibabu nyumbani kwake huko Johannesburg, na madaktari wamemueleza kuwa wanaimani sauti ya Madiba itarejea na kuweza kuongea.
Mwezi wa Septemba Mandela alirudi nyumbani baada ya kulazwa hospitali mjini Pretoria kwa karibu miezi mitatu, akitibiwa ugonjwa wa mapafu.
Serikali ya Afrika Kusini imesema hali yake bado ni ya kutia wasi wasi na wakati mwingine hubadilika.
No comments: