» » » Rais Barack Obama kwenda Afrika Kusini kuhudhuria mazishi ya Mandela Akiongozana na Mke Wake Wakiambatana na Maraisi Wastaafu, Bill Clinton na George Bush

Ikulu ya Marekani imetangaza kuwa Rais Barack Obama na mkewe First Lady Michelle, watasafiri kwenda Afrika Kusini wiki ijayo kutoa heshima zao za mwisho kwa Nelson Mandela aliyefariki dunia Ijumaa (December 5).


Rais wa zamani wa Marekani George W.Bush na mkewe Laura, pia wametangaza kuambatana na Obama, mkewe na mabinti zao katika Air Force One, kwenda Afrika Kusini kuhudhuria tukio la kumuaga na kutoa heshima za mwisho kwa Mandela.

Clinton na Madiba

Bill Clinton aliyekuwa Rais wa Marekani katika kipindi ambacho Mandela pia alikuwa madarakani, pamoja na mkewe Hillary pia watakwenda Afrika Kusini.

Viongozi wengine wa kimataifa wanaotarajiwa kwenda Afrika Kusini ni waziri mkuu wa Uingereza David Cameron, ambaye ataambatana na Prince Charles.

Huu ni uwanja wa mpira wa Johannesburg utakaotumika kwa shughuli ya kumuaga Tata Mandela.

Kwa mujibu wa ratiba ya kuelekea siku ya mazishi, tukio kubwa la kwanza litakuwa ni December 10, ambapo ‘memorial service’ itafanyika katika uwanja wa mpira Johannesburg, wenye uwezo wa kubeba watu 94,000 uliotumika katika fainali za kombe la dunia 2010, ambapo maelfu ya watu watapata nafasi ya kumuaga Mandela.

Utaratibu wa maandalizi ya mazishi ya mzee Mandela uliandaliwa zaidi ya mwaka mmoja uliopita, kipindi ambacho afya yake ilipoanza kuwa mbaya, hii ni kwa mujibu wa The Guardian ambayo inasemekana kuwa na nakala yake.

Serikali ya Afrika Kusini imesema mazishi ya Mandela yatafanyika Jumapili ya wiki ijayo (December 15), katika kijiji alichokulia cha Qunu.

SOURCE: MAIL ONLINE 



Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply