» » Taarifa Juu ya Ndege Iliyotua Arusha Kimakosa

Shirika la ndege la Ethiopia, Ethiopian Airlines jana limetoa maelezo kuhusu ndege yake namba ET-815 aina ya Boeing 767-300 iliyokuwa ikitokea Addis Ababa kwenda Kilimanjaro Desemba 18 na kutua katika uwanja wa ndege wa Arusha badala ya KIA kama ilivyokuwa imekusudiwa.

Wakitafakari Juu ya Kuitoa Ndege Hiyo Iliyokuwa  kwenye udongo ilipokuwa imenasa

Taarifa iliyotolewa kupitia website ya ETHIOPIAN AIRLINES inasema kuwa, kulikuwa na ‘miscommunication’ kati ya waongoza ndege (control tower) wa uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA) pamoja na marubani wa Ethiopian Airlines, na kusababisha kutua uwanja wa Arusha badala ya Kilimanjaro kama ilivyokusudiwa.

Shirika hilo limesema kuwa ndege hiyo ilikuwa na mafuta ya kutosha kufika kule walikotakiwa kwenda tofauti na ilivyoripotiwa, na abiria wote na wafanyakazi wa ndege hiyo hawakudhurika na walipelekwa kuendelea na safari zao walikokuwa wakielekea, pia ndege hiyo haikupata uharibifu wowote.

Nayo Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania jana Desemba 19, imetoa taarifa ya ufafanuzi juu ya tukio la ndege ya Ethiopian Airlines iliyotua juzi katika uwanja wa ndege wa Arusha badala ya KIA.




Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply