» » Liverpool yainyuka Everton 4-0

Klabu ya Liverpoool inaendeleza kampeni yake ya kutaka kuwa miongoni mwa timu nne bora katika Ligi Kuu ya England baada ya kuichachawiza Everton mabao 4-0 katika mchuano wa katikati ya juma ulioandaliwa Jumanne katika uwanja wa Anfield.



Mechi hiyo ilitajwa kama muhimu zaidi kuwahi kushirikisha pande hizo mbili baada ya kipindi cha miaka 30.



Liverpool ilitangulia kuzibusu nyavu za Everton mapema kuvuna mabao matatu; moja kupitia mkwaju wa kichwa kutoka kwa Steven Gerrad na huku Daniel Sturrige akifuma mabao mawili dakika tatu baadaye..

Everton ilipata pigo baada ya mshambulizi wa kutegemewa Romelu Lukaku kuondoka uwanjani juu ya machela baada ya kupata jeraha la kiwiko cha mguu. Aligongwa vibaya na Gareth Barry alipokuwa akijaribu kumnyima Steven Gerrard fursa ya kufunga bao.



Rodgers apongeza "juhudi kuu" za Liverpool

Ushindi huo mnono wa Liverpool tangu November 1982 umekiwezesha kikosi hicho cha Brendan Rogers kujipiga kifua juu ya matumaini ya kulidaka taji la ligi kuu. Brendan Rogers amesifu juhudi kubwa za wachezaji wake.

Katika matokeo ya mechi nyinginezo Manchester United iliishinda Cardiff mabao 2-0, Norwitch City na New Castle United zikatoka sare ya kutofungana, nao viongozi wa ligi Arsenal wakapata pigo katika kampeni yao kwa kulazimishwa kutoka sare ya mabao 2-2 ugenini dhidi ya Southampton.



Swansea iliichabanga Fulham 2-0, Crystal Palace 1 Hull 0 na Liverpool.

Leo Jumatano Manchester City itashuka dimbani ugenini kutafuta alama za kushika usukani kwenye jedwali dhidi ya Totteham Hotspurs, Aston Villa watamenyana na West Brom, Chelsea itaialika West Ham, Sunderland itaikaribisha Stoke.

Source: bbc

Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply