» » » Ben Pol Atisha, Atoa album Mpya yenye nyimbo 20 kupatikana Mtandaoni

Mkali na Mwimbaji wa R n B Ben Pol jana (February 11) ameachia single yake mpya kwa mwaka huu iitwayo ‘Unanichora’ ambayo kamshirikisha rapper wa kundi la Weusi Joh Makini, ambayo imeambatana na album yake mpya itakayopatikana mtandaoni.



Ben Pol amesema licha ya changamoto ya soko ilivyo kwa hivi sasa, ameamua kuipeleka album yake katika platform za mtandaoni ambapo tayari inapatikana katika mitandao ya iTunes, Amazon, Spotify, Shazam, Beatsmusic, Xbox music na Google play ambapo inauzwa kwa dola 9.99 katika mitandao hiyo.



Taarifa iliyosambazwa kwa njia ya e-mail sambamba na wimbo wake mpya ‘Unanichora’ imeongeza kuwa mashabiki wa Ben Pol watakaohitaji album hiyo wanaweza kununua kwa njia ya M-Pesa 0764 905 470 na pia Tigo Pesa 0715 744 911, kwa kutuma shilingi 10,000 na kupatiwa link kwaajili ya kudownload nyimbo zote ishirini.

Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply