MSANII nyota wa muziki wa kizazi kipya, Estelinah Sanga maarufu kama Linah, anadaiwa kupewa ujauzito na kijana mmoja wa Kihindi anayejulikana kwa jina moja la Nagar.
Estelinah Sanga 'Linah'.
Chanzo cha uhakika kimeliambia gazeti hili kuwa msichana huyo aliyeibukia kutoka kituo cha kukuza vipaji cha THT, amekuwa karibu na Mhindi huyo anayedaiwa kuishi Mbezi jijini Dar es Salaam kwa muda mrefu sasa na kwamba mimba hiyo imeonekana kumfurahisha sana msanii huyo.
“Huyu Nagar ni mpenzi wake wa muda mrefu na inaonekana hii mimba ameipenda sana. Kila siku anamsifu huyo mpenzi wake,” kilisema chanzo hicho kilichodai kuwa wawili hao wamekuwa wakiambatana pamoja katika sehemu mbalimbali za starehe.
Linah alikutana na mdosi huyo katika harakati zake za kimuziki na kwamba jamaa ameoza mno kwa binti huyo, mkali wa albamu ya Atatamani.
Linah alipopigiwa simu mara ya kwanza hakupokea, lakini baada ya kutumiwa ujumbe mfupi wa maneno na kuulizwa kuhusu suala hilo, alipiga simu na kukanusha vikali tuhuma hizo.
“Nani kakwambia kama nina mimba? Hakuna kitu kama hicho, hayo ni maneno ya watu wanasambaza mtaani, mimi hata sijui wananitaka nini,” alisema.
Alipoulizwa kama hata yeye amewahi kusikia habari hizo, alisema anazisikia na kusisitiza kuwa siyo za kweli. Lakini alipotakiwa kusema kama anamfahamu Nagar, alimtaka mwandishi kuachana na habari hizo.
“Wewe si umeuliza habari za mimba? Sasa hayo mengine yanatoka wapi, ulichotaka kujua nimekujibu, hayo mambo mengine achana nayo,” alisema bila kufafanua zaidi.
Source:GlobalPublishers
Tunaomba Maoni yako Hapa :
Category: celebrity News Gossips Linah
Related Posts
Fid Q amzunguzia mama wa mtoto wake Fidelie
Rapper Fid Q amesema ni mapema sana kuzungumzia masuala ya ndoa na mpenzi wake kutoka Jamhuri ya Cze...Read more »
26Sep2015Kajala Ammwagia Zari Minoti!
KIMENUKA tena! Katika kile kinachoonekana kama ni kejeli kwa shosti wake wa zamani, ambaye sasa pic...Read more »
25Sep2015Picha: Tiffah ni Photocopy ya Baba yake Diamond Platnumz
Tiffah, mtoto wa Diamond Platnumz aliyezaa na mpenzi wake wa Uganda, Zari the Bosslady ni kama photo...Read more »
25Sep2015Je Umeshawahi Kujiuliza Kama Kuna Ugomvi Wowote Kati ya Lulu Michael na Wema Sepetu...? Lulu Afunguka Haya
KAMA unafikiri kuna ugonvi kati ya waigizaji maarufu nchini, Elizabeth Michael, ‘Lulu’ na Wema Sepet...Read more »
25Sep2015Dk. Cheni Afunguka Kumuoa Lulu!
Tangu wakati ule msanii maarufu wa filamu, Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ aamue kupambana kumsaidia Eliza...Read more »
25Sep2015Mama wa Diamond Aongelea Kuhusu Mjukuu wake Kuwa si Mtoto wa Diamond
Weekend iliyopita mtoto wa Diamond na Zari aitwaye Tiffah alitimiza siku 40 na sura yake kuonyeshwa ...Read more »
25Sep2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments: