Arsenal waliokuwa nyumbani katika Uwanja wao wa Emirates wamemaliza mchezo wakiwa 10 baada ya kipa wao Wojciech Szczesny kumchezea rafu wimba wa Bayern Munich, Arjen Robben aliyekuwa anaelekea kufunga bao.
Baada ya rafu hiyo, Szczesny alizawadiwa kadi nyekundu na kuamriwa ipigwe penalti langoni mwa Arsenal japo David Alaba aliikosa.
Mechi ya leo imeshuhudia timu zote mbili zikikosa penalti ambapo ya Arsenal imekoswa na Mesut Ozil na ya Munich ikikoswa na David Alaba.
Wafungaji mabao ya Munich walikuwa Toni Kroos na Tomas Muller.
Wachezaji wa Bayern Munich wakishangilia bao lao la kwanza.
Hekaheka wakati wa mtanange huo.
Mchezaji wa Arsenal, Mesut Ozil naye akikosa mkwaju wa penalti kipindi cha kwanza.
... Szczesny akizawadiwa kadi nyekundu.
Wojciech Szczesny akijaribu kumzuia Arjen Robben bila mafanikio.
No comments: