Ile kesi iliyokuwa ikisubiliwa na maelfu ya watanzania, Kesi inayomkabili msanii wa filamu Elizabeth Michael ‘Lulu’ dhidi ya msanii mwenzake marehemu Steven Kanumba imeunguruma Jumatatu hii katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam huku mtuhumiwa akikiri baadhi ya mashtaka.
Lulu alikiri mbele ya Jaji Rose Temba kuwa alikuwa na uhusiano wa mapenzi na marehemu Steven Kanumba na kwamba walikuwa na ugomvi, lakini alikana mashtaka ya kumuua bila kukusudia.
Mbali na kukiri kuwa na uhusianano wa mapenzi, muigizaji huyo pia alikiri kuwa baada ya tukio hilo alitoka nje ya chumba walichokuwepo na kwenda kumwambia mdogo wake marehemu Kanumba, Setti Bosco kuwa Kanumba ametangulia mbele ya haki.
Akisoma hati ya mashtaka, Wakili Mwandamizi wa Serikali, Monica Mbogo, alidai kuwa Aprili 7, mwaka 2012, Sinza Vatikani, Mkoa wa Dar es salaam, mshitakiwa alimuua bila kukusudia Stevin Kanumba.
Wakili Kombo, alidai kuwa pamoja na mambo mengine, marehemu Kanumba baada ya kufa, mwili wake ilipelekwa hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo majibu yanaonyesha kwamba kifo chake kimesababishwa na uvimbe ndani ya ubongo.
Upande wa serikali una mashahidi watano pamoja na vielelezo wakati upande wa utetezi pia unatarajia kuwa na mashahidi watano na vielelezo.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi hapo watakapojulishwa na mahakama tarehe ya kusomwa kwa shitaka lake la kuua bila kukusudia.
Lulu akiwa Dk Cheni mahakamani

Source:GlobalPublishers
No comments: