» » Wajue Celebrity Vijana wenye nguvu Tanzania

Siku hizi ni tofauti kabisa na zamani ambapo tumezoea kuona watu wazima/wazee peke yao ndio watu wenye uwezo mkubwa na nguvu sana kwa hapa Tzee,siku zinavyozidi kuendelea mambo yanazidi kubadilika na siku hizi vijana ndio watu wanao-hustle juu chini kuweza kupata success hata zaidi ya wazee wao waliotangulia,kwa hapa Tzee tumeweza kupata baadhi ya vijana maarufu ambao ni most powerful na wenye influence kubwa kwa vijana wenzao.


Endelea kupata Habari Zaidi za Kila siku Kutoka BONGO61.COM  Kwa Kijiunga Hapa Buree!.


DIAMOND PLATNUMZ

Jina lake halisi ni Naseeb Abdul,so far ni msanii anayelipwa zaidi kuliko msanii yeyote wa bongo fleva hapa Tzee,na kuongoza kulipwa zaidi katika show zake za nje na ndani ya nchi.ukimuongelea Diamond platnumz hivi sasa Africa lazima utakuta idadi flani hivi ya watu wanamfahamu msanii huyu na hiyo ni mbali na huko ulaya na kwingineko duniani,ameweza kufanya kazi zake za muziki na wasanii wakubwa duniani na kuweza ku-share stage moja na wasanii akiwemo rick ross,Ludacriss ,Psquare na wengine wengi,mbali na muziki pia ni ambassador wa cocacola zero,goodwill ambasador wa malaria na ni moja ya wasanii wanaosaidia na kujitolea katika shughuli mbalimbali za kusaidia jamii.

Endelea kupata Habari Zaidi za Kila siku Kutoka BONGO61.COM  Kwa Kijiunga Hapa Buree!.



FLAVIAN MATATA

Kutoka mshindi wa kwanza wa miss universe Tanzania mwaka 2007 na kwenda kuiwakilisha tanzania mwaka huo huo,Flaviana aliweza kuingia kwenye top 15 , kuingia nusu fainali na baadae kushika nafasi ya Sita na ndiye aliyekuwa mtanzania wa kwanza kushiriki mashindano hayo ya miss universe huku akiwa amenyoa nywele zake tofauti na washiriki wenzake,it was a game changer kwa jina la Tanzania kujulikana kuwa kuna vipaji vingi vilivyofichika.

Endelea kupata Habari Zaidi za Kila siku Kutoka BONGO61.COM  Kwa Kijiunga Hapa Buree!.

Matata ameshiriki katika matangazo mengi sana akiwa kama model,mwaka 2011 aliweza kushinda tuzo ya model of the year award ya Arise magazine ya huko nchini Lagos Nigeria,ametokea katika magazine mbalimbali duniani yakiwemo Dazed & Confused, Glass Magazine, L’Officiel and i-D Magazine. mbali na advertisement amefanya modeling ya mavazi ya brand za wanamitindo maarufu duniani kama Mustafa Hassanali, Vivienne Westwood, Tory Burch, Suno, na Louise Gray,pia kushirikishwa katika picha za kutangaza collection ya mwanamitindo maarufu duniani , Alexander McQueen katika Topshop Spring 2011 ad campaign.Flaviana matata baada ya kuchukua tuzo ya “Face of Africa” aliweza kuwasaidia wanawake wenzake na anaendelea na kampeni yake katika kusaidia wasichana waweze kwenda shule kupitia foundation yake, Flaviana foundation.amekuwa ni kioo cha wanawake na vijana wengi sana hapa Tzee.



JANUARY MAKAMBA

Huwezi kutaja list hii na kumuacha mtu huyu maarufu sana na ni role model wa vijana wengi sana hapa nchini kwa yale aliyoweza ku-achieve katika umri wake huo mdogo,unaambiwa alikuwa msaada mkubwa sana katika serilkali ya Raisi.Kikwete toka mwaka 2005,mbali na hayo aliweza kupata kiti cha ubunge kupitia jimbo lake la Bumbuli kupitia chama chake cha CCM,nafasi aliyoweza kuipata kwa asilimia 80% kati ya wapinzani wake nane,hii inaonyesha kuwa ni moja ya kijana anayeaminika sana na kupendwa sana na wananchi,huyu ni moja kati ya waheshimiwa wanaopenda ku-socialize sana na watu wa hadhi mbali mbali,na wa aina tofauti kitu kinachozidi kumfanya kukubalika sana na vijana wenzake pia kumsaidia kujua matatizo yao na jinsi yakuwapatia suluhu.


Endelea kupata Habari Zaidi za Kila siku Kutoka BONGO61.COM  Kwa Kijiunga Hapa Buree!.



HASHEEM THABEET

Jina lake halisi ni Hashim Thabeet Manka ila maarufu kama Hashim Thabeet tu,ni moja kati ya basketballer professional duniani anayeichezea timu ya Oklahoma City Thunder.ni vigumu sana kuamini kwa mchezaji maarufu wa huko NBA kutoka hapa hapa kwetu Tanzania,huyu ni moja kati ya wachezaji warefu sana maarufu katika ligi ya mpira huu wa kikapu wa huko marekani,ni moja kati ya wanamichezo wanaolipwa kuliko yeyote kutoka hapa Tanzania na hata baadhi ya nchi,za hapa east Africa,na ni moja kati ya celeb wakubwa sana hapa Tzee wanaojishughulisha sana na kazi zakujitolea kwa jamii.



Endelea kupata Habari Zaidi za Kila siku Kutoka BONGO61.COM  Kwa Kijiunga Hapa Buree!.

LADY JAY DEE

Ni moja kati ya wanawake wenye majina makubwa sana hapa mjini,ikiwa ni msanii mkubwa sana wa kike anayeheshimika kutokana na kazi zake nzuri za kimuziki, anamiliki biashara mbalimbali hiyo ni mbali kabisa na muziki unaosemekana unamuingizia hela nyingi sana,mbali na muziki pia ni mjasiliamari mkubwa sana,akiwa ni CEO wa Nyumbani Lounge ,Studios na biashara nyingine nyingi,she is a hustler.ukimuongelea lady jay dee ni msanii wa kike mwenye umaarufu na utajiri mkubwa, anapendwa na kila mtu na kukubalika sana kimuziki na nje ya mziki huu wa Bongo fleva.


ZITTO KABWE

Jina lake halisi anaitwa Kabwe Zuberi Zitto ila maarufu anajulikana tu kama Zitto Kabwe,huyu ni mmoja wa wanaharakati wanaojitahidi kutetea haki za wananchi bila kuficha lolote lile kwa hadhira,ni moja ya tunda litokalo kwenye chama cha demokrasia,pia ni mheshimiwa mbunge wa jimbo la huko kigoma,ni moja kati ya vijana wenye umri mdogo na kuweza kutikisa sana nchi haswa kwa hoja zake,umahiri wake kisiasa ndio moja ya vitu vinavyopelekea kuzidi kupendwa sana na wananchi na hasa katika swala zima la kutetea haki za wananchi,ni kijana hodari sana inapokuja kwenye swala zima la siasa.


Endelea kupata Habari Zaidi za Kila siku Kutoka BONGO61.COM  Kwa Kijiunga Hapa Buree!.


PATRICK NGOWI

Ni baada tu ya kuona kuwa kulikuwa na umuhimu wa kupata plan B ya umeme hapa Tzee,Patrick aliamua kuachana na biashara ya kuuza simu na kuanza kuingiza umeme wa solar hapa Tzee kwa mtaji mdogo tu na baadae kuzidi kukua huku wananchi kuweza kupata suluhisho la tatizo lao la umeme hasa kule kulipokosekana tumaini la kuwa na umeme,hivi ndivyo alivyoanza kujipatia umaarufu mkubwa na biashara kukua sana kupitia kampuni yake inayoitwa Helvetic Solar Contractors,kampuni iliyongezeka thamani na kufikia zaidi ya dola milioni tatu kwa mwaka,hawa ni moja kati ya vijana walioweza kutumia fursa.



OSSE GRECA SINARE

Talking about photographers maarufu sana hapa Tanzania na nje ya Tanzania,Osse is the name to be mentioned, Jina lake na kazi yake imeweza kutambulika na mataifa mbali mbali hata nje ya Tanzania,na kuweza kuongelewa na baadhi ya majarida na mitandao mikubwa sana ikiwemo Africa-vogue,fashion Ghana.com ,FAS mgazine na Msongo,si tu hapo pia ameweza kufanya interview nyingi sana na media kubwa africca ikiwa inaongelea kazi zake kwa kutambua uwezo wa kazi zake,mwaka 2012 aliweza kupikea tuzo kutoka Swahili Fashion Week tuzo ya Best Fashion Photographer,pia hujishughulisha na kazi za kusaidia jamii katika kuleta mabadiliko katika maisha ya jamii zetu za hapa Tanzania.

Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply