» » » Oscar Awards: Lupita Nyong'o anyakua tuzo za kuwa muigizaji msaidizi katika tuzo za Oscar

Kama ilivyokuwa imetarajiwa na wengi mwigizaji mashuhuri kutoka Kenya Lupita Nyong'o amenyakuwa tuzo la Oscar la mwigizaji msaidizi wa kike kwa jukumu lake la kuelezea masaibu ya Patseh katika filamu ya utumwa ya ''12 Years A slave.''


baada ya kupokea tuzo hilo lupita amesema " Haikwepi katika mawazo yangu kwamba hata dakika moja ya furaha katika maisha yangu ni shukran na maumivu makubwa kwa mtu mwingine.''

Kisha Lupita akaongeza kusema, " Na iwe ukumbusho kwangu na kila mtoto kwamba kokote unakotoka, ndoto zako ni halisi.''

Sherehe ya kutolewa kwa tuzo hizo zimefanyika mjini Los Angeles nchini Marekani.

Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Picha: Red Capet ya tuzo za Oscar 2014, Tazama Mastaa walivyovaa
»
Previous
Fast & Furious 7 kuendelea kurekodiwa mwezi April, ni baada ya kusimama ‘production’ miezi 4 baada ya kifo cha Paul Walker

No comments:

Leave a Reply