Habari kwa Ufupi :

    3:0
» » » Paul Walker kuonekana kwenye filamu mpya 'Fast and Furious 7' kwa njia ya CGI

Mashabiki wa filamu ya Fast and Furious na nyota wa filamu hiyo aliyefariki kwa ajali ya gari November mwaka jana, Paul Walker wana kila sababu ya kuifurahia teknolojia ya dijiti itakayowapa nafasi ya kuona taswira ya nyota huyo kwenye filamu mpya ‘Fast and Furious 7’.


Chanzo cha karibu na waandaaji wa filamu hiyo kimeliambia gazeti la New York Daily News kuwa waandaaji hao wamekodi waigizaji wanne ambao wanafanana umbo na marehemu Paul Walker na watawatumia kwa kutumia teknolojia ya ‘Computer Generated Imagery ‘CGI’.

Kwa kutumia teknolojia hiyo, inaweza kutengeneza sauti za Paul Walker na taswira yake kwa kutumia waigizaji hao wanaofanana nae umbo.

“Paul’s face and voice will be used on top using CGI.” Kimesema chanzo hicho.

Scenes za mwisho za filamu hiyo zimeshutiwa Atlanta, Georgia ikiwa na mastaa wengine kama Vin Diesel, Ludacris na Tyrese.

Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Nisher afunguka juu ya video mpya ya Shilole, ‘ The EXPLICIT version ni ya Internet tu! ya TV itakua Clean Version’
»
Previous
Audio: Pancho Latino aizungumzia B'Hitz na yaliyojiri, "mtu kujitoa B'Hitz hakunipunguzii chochote" ampa MRap baraka zote

No comments:

Leave a Reply