» » Waziri Mkuu wa Australia asema mabaki ya ndege ya Malaysia yameonekana

Australia inadadisi picha za Satelite za vitu viwili vinavyodhaniwa kuwa mabaki ya ndege iliyopotea ya Malaysia. Nchi hio inashirikiana na Norway, New Zealand na Marekani kutafuta mabaki hayo.


Upepo mkali na mvua zilitatiza juhudi hizo hii leo na kusababisha shughuli hiyo kusitishwa. Hata hivyo msako huo utaendelea siku leo Ijumaa.


Picha za Satelite za kinachodhaniwa kuwa mabaki ya ndege


Waziri mkuu wa Australia Tony Abbott mapema leo aliambia bunge la nchi hio kuwa picha zilizonaswa na mitambo ya Satelite ya nchi hio baharini, zilionekana kama vipande viwili vya mabaki ya ndege hiyo.

Kipande kimoja kilikuwa na urefu wa mita 24.

Bwana Tony Abbott,aliambia bunge kuwa hii ni taarifa mpya na iliyothibitishwa.

Lakini maafisa wakuu nchini Malaysia wametahadharisha kuwa mabaki hayo huenda sio ya ndege yake, ambayo ilipotea siku kumi na tatu zilizopita ikiwa imewabeba watu 239 kuelekea Beijing.

Mabaki hayo yalionekana umbali wa kilomita elfu mbili miatano Kusini Magharibi mwa mji wa Perth.

Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply