Home
»
celebrity News
»
Diamond Platnumz
» Diamond Platnumz aliandikiwa wimbo na Mzee Gurumo, ila akukabidhiwa mpaka umauti unamfika mzee gurumo
Star wa Bongo fleva Diamond Platnumz amesema kuwa siku chache kabla mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi Maalim Muhidin Gurumo hajaaga dunia alikuwa amemuandikia wimbo kama shukrani kwa kumpa zawadi ya gari mwaka jana.
Platnumz amesema meneja wake Babu Tale alimpa taarifa hiyo njema ya kuandikiwa wimbo na Gurumo lakini kwa bahati mbaya mzee Gurumo alifariki kabla hajamkabidhi wimbo huo.
“Juzi kampigia simu Tale akamwambia kuna nyimbo nimemtengenezea Diamond kwasababu kwa alichonifanyia mimi nimeshukuru sana cha kumlipa mimi sina lakini nimemuandikia nyimbo”amesema Platnumz kupitia 255 ya XXL ya Clouds Fm.
“so alikuwa anamwambia Tale kama ameniandikia nyimbo, so angependa anipatie nikamwambia sawa. Kama siku tatu hivi nyuma, jana ndio nasikia taarifa hizi so najiona kama nimechanganyikiwa hivi.”
Platnumz ameongeza kuwa mara ya mwisho kuonana na Gurumo ilikuwa ni takribani wiki tatu zilizopita baada ya mwimbaji huyo mkongwe kumsurprise kwa kuhudhuria katika show aliyokuwa anatumbuiza Diamond kwa lengo la kutaka kumwona na kumshukuru kwa zawadi ya gari aliyompatia.
“Mara ya mwisho kukutna naye nilikuwa nafanya show Coco akaja maskini ya Mungu mpaka kwenye show…kama wiki moja nyuma kama sikosei au wiki mbili. Akaja akasema nimekuja hapa kukuona, alipenyapenya hadi akaweza kufika pale…nilivyomuona anakuja ilibidi pale nikatishe show nikamsalimia kidogo halafu nikaendelea na show, halafu baadae nikawa niko nae backstage na nini nikazungumza nae.So akasema nimekuja kukushukuru sana sana sana, akasema ningependa uje nyumbani nikamwambia sawa.”Amesema Diamond.
Mwili wa marehemu mzee Gurumo umepelekwa kijijini kwake Masaki, wilaya ya Kisarawe mkoa wa Pwani kwaajili ya mazishi yanayofanyika leo.
Tunaomba Maoni yako Hapa :
Category: celebrity News Diamond Platnumz
Related Posts
Mama wa Diamond Aongelea Kuhusu Mjukuu wake Kuwa si Mtoto wa Diamond
Weekend iliyopita mtoto wa Diamond na Zari aitwaye Tiffah alitimiza siku 40 na sura yake kuonyeshwa ...Read more »
25Sep2015Picha: Tiffah ni Photocopy ya Baba yake Diamond Platnumz
Tiffah, mtoto wa Diamond Platnumz aliyezaa na mpenzi wake wa Uganda, Zari the Bosslady ni kama photo...Read more »
25Sep2015Music: Wimbo ramsi wa tuzo za Afrimma ulioshirikisha wasanii 10 akiwemo Diamond, Yvonne Chaka chaka, Vanessa Mdee…
Wasanii kutoka nchi mbalimbali za Afrika wanaowania tuzo za Afrimma wameungana kufanya wimbo rasmi w...Read more »
26Sep2015Diamond Platnumz Azua Kizaazaa Kampeni za Magufuli Bukoba....
Kundi kubwa la vijana wakigombea kumuona mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’, katika Viwanj...Read more »
25Sep2015Inasemekana hawa ndio Mastaa wa kibongo waliowazidi umri wapenzi wao
Mara nyingi tunaishia kusikia rumors tu, kuwa msanii fulani amemzidi umri mpenzi wake na mara nyingi...Read more »
24Jun2014Music: Linah ft Diamond Paltnumz - Kizai Zai
Sikiliza wimbo Mpya kutoka kwa Mwanadada Linah akimshirikisha Diamond Platnumz ngoma inaitwa “Kizai ...Read more »
20Jun2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments: