Habari kwa Ufupi :

    3:0
» » » Hali ya Michael Schumacher yaimarika

Bingwa wa zamani wa mbio za magari ya langalanga ya F1, Michael Schumacher ameanza kuonyesha hali ya kupata fahamu baada ya miezi kadha ya kuwa katika hali ya kutojitambua.




Wakala wake Sabine Kehm amesema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari amesema Schumacher "anaendelea vizuri", akisema kwamba wana "uhakika"wa kupona kwake.

Madaktari nchini Ufaransa wanafanya jitihada za kumwondoa katika hali ya kutojitambua, bingwa huyo mara saba wa F1.

Mjerumani huyo mwenye umri wa miaka 45-alipata majeraha makubwa ya kichwa baada ya ajali wakati akiteleza kwenye barafu katika milima ya Alps nchini Ufaransa Desemba 29,2013.

"Tuko pamoja naye katika kipindi hiki kigumu kwake, sisi na timu nzima ya madaktari na wauguzi wa hospitali ya Grenoble," amesema Bi Kehm.

Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Tanzania yalifungia shirika la Sisi kwa Sisi, Chanzo ni kusaidia ndoa za Jinsia Moja
»
Previous
Matokeo ya Mechi kati ya Manchester United na Barca April 9 2014

No comments:

Leave a Reply