Kwa jinsi wimbo huo ulivyohit ni wazi kwamba ungeweza kuwa kati ya nyimbo ambazo zingechaguliwa na watumiaji wengi wa simu za mkononi kuwa sehemu ya miito ya simu zao lakini wimbo huo haupo katika biashara hiyo.
Rich Mavoko ameiambia tovuti ya Bongo61 sababu zinazopelekea kutokuwepo kwa wimbo huo katika biashara ya miito ya simu.
“Nyimbo zangu nyingi za mwanzo zimekuwa kwenye ringtone na sijapata faida yeyote kwenye ringtone. I swear to God sijapata faida yoyote kwenye ringtone za kibongo wala sioni umuhimu wa ringtone kama tunavyonyonywa wasanii. Mimi nitakuwa msanii wa kwanza wakisema tunatoa hiyo system…kwa sababu sipati faida yoyote zaidi ya kupata stress. Yaani kumfuata mtu kuanza kumwambia malipo yangu…mimi nimeimba halafu wewe unisumbue mimi. Na unapokuja na makaratasi yako kusaini unaniomba mwanangu utapata asilimia hizi, sipati asilimia zozote. Roho Yangu siwezi kuiuza huko, inabidi niuze nyimbo kama nyimbo.”
No comments: