» » » Kala Jeremiah: Wale Wale remix imejitosheleza

Rapa kala Jeremiah, baada ya kutoka na remix ya Ngoma yake ya Wale Wale wiki hii, kazi ambayo imepokelewa vizuri sana na mashabiki, amesema kuwa muunganiko aliojaribu kutengeneza katika ngoma hii, amemuhusisha Juma Nature, Young Killer na Ney Lee.
Rapper Kala Jeremiah
Kala amesema kuwa muunganiko wa wasanii hawa katika ngoma hii ni kutokana na lengo la kuweka ladha tatu zenye malengo makubwa kwa mashabiki wa muziki anaofanya sasa.

Kala amesema kuwa, Juma Nature amehusika katika ngoma hii kutokana na kutosheleza kwake katika kazi hii nzima, huku akiweka wazi kuwa tokea anafanya "Origional Version" ya kazi yenyewe alikuwa na wazo la kumshirikisha msanii huyu mkongwe, na pia Young Killer akisimama katika kazi hii kuvuta zaidi kizazi kipya katika game ya michano, wakati Ney Lee akiwa anasimama kama kionjo cha sauti tamu kwaajili ya wapenzi wa ladha katika muziki wa Bongo Flava.

Kala amesema kuwa, video ya kazi hii pia ni moja ya kazi ambazo zimemchukua muda zaidi kufanya na kumpatia uzoefu mpya kabisa ikiwa ni pamoja na kuona muziki wake ukikua.

Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply