![]() |
Helkopta iliyokuwa imebeba baadhi ya viongozi na kupata ajali hii leo jijini DSM. |
Wengine waliokuwemo ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Mecky Sadiki pamoja na wajumbe wa kamati ya maafa, ambapo hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa katika ajali hiyo na walipelekwa hospitali kuchunguzwa iwapo wamepata madhara na kuruhusiwa.
Tukio hilo limetokea leo Jijini Dar es Salaam katika uwanja wa ndege wa jeshi wa Ukonga majira ya saa Tano asubuhi, ambapo viongozi hao walipokuwa wakijiandaa kupaa na helkopta hiyo na ndipo ilipopata hitilafu baada ya kuruka juu kidogo na kuanguka.
No comments: