Gari lake lililompeleka Global kufanya timbwili.
Kwa mujibu wa Wema, magazeti ya Global yamekuwa yakimwandika vibaya yeye na mpenzi wake Diamond huku akitolea mfano wa habari iliyomhusu yeye na mwigizaji Aunt Ezekiel baada ya kunaswa kwa picha zao zilizoashiria vitendo vya usagaji.
Wema akiwa ndani ya ofisi za Global na sura ya 'kuua mtu', mkononi akiwa na gazeti la Ijumaa Wikienda lenye stori: DIAMOND ATAMANI USHOGA. Kushoto ni mpambe na mfanyakazi wake Petit Man Wakuache.
“Hivi mnajua mimi ni chizi? Kwa taarifa yenu mimi ni chizi zaidi ya machizi wote, ohooo!”
MLINZI ATONYWA, ATIA TIMU
Baada ya hali kuwa tete, mlinzi wa geti kuu alipigiwa simu ya mezani na kujulishwa juu ya Wema kusababisha kazi kusimama ambapo alifika haraka tayari kwa kumtoa nje kwa hiyari yake au lazima.
Katika purukushani hiyo, Wema alionesha udhaifu wa kumudu varangati pale alipotumia gazeti aliloshika kumpiga nalo mwandishi Imelda, jambo lililodhibitiwa kama Waasi wa M23 wa Kongo walivyodhibitiwa na Majeshi ya Umoja wa Mataifa, akatolewa nje.
Hata hivyo, uongozi wa Global uliwasiliana na Polisi wa Kituo cha Kijitonyama ‘Mabatini’, Dar ambao walifika na kumkuta Wema na timu yake wakiwa wamepoa mlangoni, wakaambiwa timbwili limetulia hivyo wakatimua zao.
"Mimi ni chizi, nakwambieni mimi ni chizi zaidi ya machizi wote"....Wema alikuwa akifoka mwanamke!
Katika kuhoji huko, mhariri kiongozi alijaribu kumtuliza Wema ambaye alikuwa kama amewehuka: ”‘Wema tuelewane, eleza shida yako kwa utaratibu kwani hakuna ofisi isiyokuwa na utaratibu.”
WEMA NA IMELDA
Katika kumtafuta Imelda kwa macho kwa sababu chumba cha habari ni kikubwa huku akionywa na wahariri kwamba atulize mzuka kisha aeleze shida yake, Wema alimuona Imelda akitoa maelezo kwa Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa ya Global, Oscar Ndauka kuhusu habari aliyokuwa ameifuatilia.
“Kwa nini mnafuatilia maisha yangu? Kila siku mnaniandika na Diamond. Kwa nini Imelda unaniandika kuwa mimi msagaji?”
Baada ya kugundua kadi ya kamera ipo chini ya ulinzi wa Global, Wema alitaka kulianzisha tena akidai hawezi kuondoka hadi apewe kadi hiyo lakini uongozi uliweka ngumu. Baadaye aliondoka kimyakimya. Wakati huo wapambe wake walishaondoka kitambo.
No comments: