» » » Hawa ndio waliosababisha Diamond Platnumz kuanza kuvaa sketi stejini.

Wanajiita Twinz fashion, Unaweza dhani kuwa Diamond Platnumz huwa anaagiza pamba zake nje ya nchi hivi, kama states na kuzivaa hapa bongo kama ilivyo kwa wasanii wengi wa Bongo Fleva, haswa pale anapopata umaarufu.



 Ila Twins Fashion  ndio wanahusika asilimia kubwa ya pamba azitupiazo Diamond Platnumz. Ilishtusha watu wengi pale Diamond alipohudhuria tuzo za Kili huku yeye pamoja na ma-dancers wake wakiwa wamevalia sketi fulani hivi fupi pamoja na suruali, huku akiwaacha mamia ya watu waliohudhuria sherehe hizo mdomo wazi nakunong’onezana, kumbe zile ni trend mpya hapa town, na twinzfashion ndio waliohusika kumvisha Platnumz pamoja na dancers wake wote sketi nyeupe.
Wanajiita Twinz fashion










Sio diamond tu, wasanii wengi wameonekana wakipendelea ubunifu wa hawa vijan, na mara nyingi huonekana wakiwa wamevalia nguo za kipekee, na waTzee wengi hudhani kuwa zimeagizwa kutoka states hivi, moja wapo ni hii ya Ommy Dimpoz, ukiangalia haraka haraka ni vigumu kuamini kuwa kama ubunifu huu ni wa hapa hapa Bongo,kutokana na ujuzi uliotumika katika kubuni na kulitengeneza vazi hili adimu.


Wasanii wengi wakubwa hivi sasa wameanza kushtuka, na kuanza kuvaa nguo za wabunifu wa hapa hapa Tzee, kama msanii ni muhimu pale unapona kazi zako zinakubalika na wewe kuonyesha unakubali kazi za wasanii wenzako ikiwa ni pamoja na ubunifu, hii inamuweka msanii aonekane ametoka kipekee, hapo hapo unatangaza kazi ya mbunifu, ambaye naye pia ni msanii anayetumia ubunifu wake kupendezesha. Kwa hapa bongo mambo si mabaya ingawa bado tupo njiani sababu hata wasanii wetu wameanza kutoa sapoti kubwa kwa wabunifu wa hapa nyumbani, hivyo kuzidi kuonyesha uzalendo.

Twinzfashion inakutanisha vijana wawili ambao ni moja kati ya kundi kubwa la wabunifu wa hapa nyumbani,  wanaoleta mabadiliko katika industry hii yetu ya ubunifu wa mavazi, ni moja kati ya wabunifu makini sana wanaokubalika na watu mbalimbali ikiwemo wasanii wakubwa hapa Bongo na watu mbali mbali maarufu wanaofurika kuweka order ya mavazi mbalimbali kuanzia ya kiume hadi ya kike.

Hapo chini ni moja ya vazi alilowahi kulivaa Diamond Platnumz, ilimtoka kiasi cha Tsh 100,000/- ili aweze kuitinga siku hiyo.




Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply