Mtandao wa Vanguard wa Nigeria umeandika kiasi cha pesa wanachotoza wasanii wa A-list wa Nigeria kwa show moja.
P-Square – M 150 Tshs
Mapacha wa P-Square Peter na Paul ndio wasanii wanaoonekana kutoza pesa nyingi zaidi, ili watumbuize katika show wanatoza kuanzia Naira milioni 8 hadi 15, sawa na Tshs milioni 81 hadi milioni 152 kwa show moja.
D’banj – Milioni 100 Tsh
Koko Master D’Banj anatoza kuanzia Naira M6 hadi 10 sawa na Tsh milioni 60 hadi M100 kwa show.
2 Face – Milioni 60 Tsh
2 Face Idibia anatoza kuanzia Naira milioni 5- 6 ambayo ni sawa na Tsh milioni 50 hadi milioni 60 kwa show moja.
Wizkid – M 50 Tshs
Wizkid hutoza kuanzia Naira milioni 4-5 sawa na Tshs milioni 40 hadi 50 kwa show.
Flavour – M 30 Tshs
Flavour huchukua Naira milioni 3 sawa na Tshs milioni 30 kwa show
Iyanya – M 30 Tshs
Kukere master Iyanya hutoza sawa na Flavour Naira milioni 3 sawa na Tshs milioni 30
Davido – M 35 Tshs
Davido ambaye pia ameshirikishwa katika Number 1 na Diamond Platnumz, hutoza Naira milioni 3 hadi 3.5 sawa na Tshs milioni 30 hadi 35 kwa show.
Tiwa Savage – M 25 Tshs
Tiwa Savage ambaye zamani akiwa Marekani alianza kwa kuwa backup singer kwa wasanii wakubwa kama Mary J na wengine, yeye huchaji Naira milioni 2.5 sawa na tshs milioni 25 kwa show.
No comments: