Rapper wa Arusha, Joh Makini ana ndoto kubwa na amejipanga vizuri kuhakikisha kwamba sio tu anafika level za kimataifa bali anawafunika hata wale walioko kwenye level hizo akizitimiza ndoto zake.
Joh aliwapa zawadi watu waliohudhuria uzinduzi wa video ya wimbo wa Weusi ‘Gere’, kwa kuwasikilizisha wimbo wake ambao haujatoka alioupa jina la ‘I See Me’, wimbo ambao ni dhahiri kwamba utafanya vizuri utakapoachiwa rasmi.
Katika wimbo huo uliotayarishwa na Nahreel, Joh Makini anasikika akielezea ndoto zake na anapojiona kwenye game akifika mbali, “I see me Internationally, I see me overtaking Wale…” anarap Joh Makini.
No comments: