Song: mguu pande mguu sawa
Artist: stamina ft walter chilambo
Studio: one love fx
Producer; tiddy hotter
Song writer: stamina (verse),walter (choruss)
Intro;stamina
Yeaaah,,,u know what tiddy
One love fx again men
Iz moro town in da house
Shorwebwenzi on this one
Vers 1(stamina)
Peleka kitanda batani,kama unapenda ukeshe bar/
Sista duu muda hausimami,hata uivulie nguo saa/
Ishi kiushujaa,kama umepanga kambi ya jeshi/
Kati ya maarufu na star,maarufu anaongoza kwa deshi/
Ewe raisi wa wanyama,fanya sensa usisahau/
Mfuasi aliyesaliti chama,huku mjini bonge la nyau/
Tunza bible sio irizi,ufalme wa mbingu hauna fensi/
Ndo maana akifaga mzinzi,mazishi hatufanyi gesti/
Chagua kilicho best,kati ya copy na kupaste/
Je Yule aliyefeli maisha na class alifeli test?/
Hakuna demu anayejiuza,hicho ndo nikijuacho/
Nachojua wanakodisha,unatumia huondoki nacho/
Bitozi msaka mchumba,usiforce unapotemwa/
Piga goti kwa muumba,ikibidi akuumbe tena/
Mguu mmoja pande,mwingine urudishe sawa/
Hiyo ndo ishara ya kiafande,ya kuweka mambo sawa/
Chorus(walter chilambo)
Naamini kama nyuma ulikosea rudi
Weka mambo sawa na plan b
Unaweza fanya bora zaidi (muda bado)
Mguu pande(mojaaaaa)mguu sawa(mojaaaaa)
Nyuma geuka(moja mbili tatu mojaaa)…..x2
Mguu pandeeee(mojaaaaaa)mguu sawa(mojaaaa)
Nyuma geukaaaaaa.
Verse 2(stamina)
Mjini wanyama kibao,cha ajabu wanakula unga/
Mawazo ya vichwa vyao,dingi afe warithi nyumba/
Ewe kengeza,chunga usimcheke chongo/
Cha msingi muombe ebeneza,akupe vision yenye michongo/
Saka chaka kila sehemu,maana pesa ina machale/
Nyie mnaowinda mademu,hivi mna nyota ya mshale?/
Mnyamazie mshenzi,ukimjibu tu anatuna/
Hadi shoga nae ana mpenzi?,kweli madem mna huruma/
Mziki umejaa stress,ambazo haziishagi kwa pombe/
Mastar wamewekeza desi,wanakufa hawana hata ng’ombe/
Underground chondechonde,usiache shule kisa mziki/
Usuperstar una mabonde,na miteremko ya dhiki/
Yesu anarudi lini?,hilo swali ndo ujiulize/
Sio stamina utaoa lini,nitajibu tu niko bize/
Mguu mmoja pande,mwingine urudishe sawa/
Hiyo ndo ishara ya kiafande,ya kuweka mambo sawa/
Chorus(walter chilambo)
Naamini kama nyuma ulikosea rudi
Weka mambo sawa na plan b
Unaweza fanya bora zaidi (muda bado)
Mguu pande(mojaaaaa)mguu sawa(mojaaaaa)
Nyuma geuka(moja mbili tatu mojaaa)…..x2
Mguu pandeeee(mojaaaaaa)mguu sawa(mojaaaa)
Nyuma geukaaaaaa.
Vers 3(stamina)
Usitupe mayai kiholela,zalisha ili uache chata/
Maisha baiskeli ya delela,ukiinama chako unapata/
Kumpa kibogoyo mnofu,kisa nyama bei aghali/
Ni sawa na kumteta kipofu,huku kifikra anaona mbali/
Hakuna zali la mentali,kwenye sayari ya kupendwa/
Mlevi mnywa safari,je unajua unapokwenda?/
Acha mashauzi,sista duu genge linalipa/
Ujanja sio kwenda south,au china ili ukawe striper/
Mapenzi ni kutendwa,mpendaji jiamini/
Sharo ukiona unapendwa,ujue una nyota ya ukimwi/
Ni sawa na uote,usiku una kiss na jini/
Halafu uamke ujikute,una lips stick kwenye ulimi/
Unahitaji akili,sio mashavu yenye dimpoz/
Mwanaume jasiri,hajichubui kisa ana pimpoz/
Mguu mmoja pande,mwingine urudishe sawa/
Hiyo ndo ishara ya kiafande,ya kuweka mambo sawa/
Chorus(walter chilambo)
Naamini kama nyuma ulikosea rudi
Weka mambo sawa na plan b
Unaweza fanya bora zaidi (muda bado)
Mguu pande(mojaaaaa)mguu sawa(mojaaaaa)
Nyuma geuka(moja mbili tatu mojaaa)…..x2
Mguu pandeeee(mojaaaaaa)mguu sawa(mojaaaa)
Nyuma geukaaaaaa.
No comments: