Rais wa Malawi, Joyce Banda amesema anaufuta uchaguzi mkuu uliofanyika wiki hii nchini humo ambao naye alikuwa anagombea kwa kile alichokisema ni kasoro za upigaji kura.
Awali Ms Banda alisema uchaguzi huo ulikuwa umekumbwa na udanganyifu, watu kupiga kura mara mbili na computer-hacking. Amesema kura mpya zitapigwa ndani ya siku 90 lakini yeye hatogombea tena. Jana jioni tume ya uchaguzi ya Malawi, (MEC) alisema mpinzani wake Peter Mutharika alikuwa amepata asilimia 42%, baada ya 30% kuhesabiwa.
Joyce Banda alikuwa na 23%.
No comments: