Unknown
11 years ago
Mume wa muimbaji wa injili Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha ambaye pia ni muimbaji anatafutwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kumbaka shemeji yake mwenye umri wa miaka 17.
Kwa mujibu wa Global Publishershers, mwanaume huyo anasakwa na jeshi la polisi baada ya shemeji yake kuripoti katika kituo cha polisi Jumatatu wiki hii majira ya mchana na kufungua mashitaka dhidi ya mwanaume huyo akidai kuwa alimmbaka kwa nyakati tofauti katika siku mbili (Ijumaa na Jumapili) ya wiki iliyopita nyumbani kwa Mbasha, Tabata-Kimanga, Dar es Salaam.

Imeelezwa kuwa mlalamikaji alifanyiwa kitendo hicho Jumamosi sebuleni kwa Mbasha, na Jumapili ndani ya gari la mlalamikiwa na kwamba kutokana na maumivu makali aliyosababishiwa aliamua kuripoti katika kituo cha polisi na kufungua kesi yenye Kumbukumbu Na. TBT/RB/3191/2014 na ya Jalada la Uchunguzi Na. TBT/IR/1865/2014.
Taarifa hizo zimeeleza kuwa kulikuwa na ugomvi mkubwa kati ya Flora na mumewe hali iliyomsababiha Flora kuondoka nyumbani na kuishi hotelini na nafasi hiyo mumewe aliitumia kufanya tukio hilo.
Global Publishers imeeleza kuwa ilizungumza na mlalamikaji kwa njia ya simu na alithibisha kufanyiwa kitendo hicho na mume wa Flora na kueleza kuwa tayari wameshatoa taarifa polisi.
Jumapili (May 25) ambayo mlalamikaji anadai alibakwa ndani ya gari na Emmanuel, Flora Mbasha alipost kwenye ukurasa wake wa Facebook picha mbalimbali za matukio mbalimbali akiwa na mumewe, huku picha ya mwisho ikimuonesha mume wake huyo akiwa nje ya hospitali ya kanisa huko Haydom, Mbulu (Haydom Lutheran Hospital) na kuandika ‘Haydom’.
Hata hivyo, tangu kuwepo na tuhuma hizo mwimbaji huyo wa kike hajapost chochote kwenye Facebook.
Jeshi la polisi bado halijatoa tamko rasmi kuhusu tukio hilo.
Tunaomba Maoni yako Hapa :
Category:
Flora Mbasha
Gossips
News
Related Posts

Aunt Ezekiel aelezea tuhuma za kutoka kimapenzi na Dancer wa Diamond Plantumz
Mwigizaji wa filamu nchini Aunty ezekiel ameelezea tuhuma zilizozogaa siku kadhaa zilizopita kuwa ...Read more »
08Aug2014
Wnafunzi hawa wakutwa wakifanya ngono kweupeeee...
Baadhi ya madenti wa vyuo vikuu mbalimbali jijini Dar es Salaam, wameoza kwa matukio machafu ya ngon...Read more »
07Aug2014
HII NDIO DAWA YA TIBA YA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME....
Suala la nguvu za kiume kwa sasa limeshakuwa ishu kubwa kwa vijana wengi wa sasa,kwa utafiti uliofan...Read more »
07Aug2014
Picha /Video:Hii ndio Ajali iliyotokea Makongo yaua watu 18
Ajali ajali! Gari aina ya Toyota Coaster inayofanya safari zake kati ya Ubungo na Tegeta jijini Dar ...Read more »
21Jun2014
Walioshambulia Kenya si Al Shabaab, 'Uhuru Kenyatta'
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amesema mashambullio yaliyotokea katika mji wa Mpeketoni, Pwani ya Ken...Read more »
17Jun2014
Picha: Hvi ndivyo jinsi Director na Kipenzi cha wengi Geogre Tyson alivyoagwa
Mchana wa leo mamia ya Watanzania walifurika katika viwanja vya Leaders Club kuuaga mwili wa Directe...Read more »
04Jun2014
Hivi ndivyo William Mtitu anavyomtuhumu Flora Mbasha, kuwa yeye ndio chanzo cha mume wake kwenda jela
Mongozaji wa filamu za kitanzania maarufu kama Bongo Movies, William Mtitu amemshushia lawama muimba...Read more »
19Jun2014
Mume wa Flora Mbasha apanda Kizimbani, akana kubaka arudishwa tena keko
Mume wa mwimbaji Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha (32), amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala ...Read more »
17Jun2014
Video: Baada ya Ukimya wa Muda, Flora Mbasha afunguka kisa kizima, Mtazame hapa
Muimbaji wa Injili Flora Mbasha amefunguka kuhusu kisa cha mume wake, Emmanuel Mbasha kumtishia kumu...Read more »
11Jun2014
Haya ndiyo anayoyasema mume wa flora Mbasha juu ya kesi inayomkabili ya kumbaka Shemeji yake
Emmanuel Mbasha, ambaye ni mume wa mwimbaji nguli wa nyimbo za Injili, Flora Mbasha amejitokeza hadh...Read more »
03Jun2014
Audio: Mume wa Flora Mbasha azungumza yote, kubaka na mengineyo msikilize hapa
Tunaomba usikilize hii audio Mume wa Flora Mbasha akiomba msamaha na akifichua mambo magumu mazito y...Read more »
03Jun2014
Exclusive Audio: Jeshi la Polisi lathibitisha kupokea tuhuma za ubakaji dhidi ya mume wa Flora Mbasha
Jeshi la Polisi limethibisha kupokea tuhuma za ubakaji dhidi ya mume wa mwimbaji wa injili Flora Mba...Read more »
30May2014
No comments: