Ile orodha ya wasanii watakaoshiriki kwenye Kili Music Tour 2014 imetangazwa leo. Kwa mwaka huu zaidi ya wasanii 30 watashiriki katika ziara hiyo kwenye mikoa zaidi ya 10 nchini na itakayoanza ambao Mei hadi Septemba 2014. Wasanii hao ni pamoja na Diamond, Ommy Dimpoz, Linex, Proffesor Jay, Izzo Biznes, Kala Jeremiah, Fid Q, Snura, Weusi, Ben Pol, Mzee Yusuph, Shilole na Mwasiti.
Hawa ni baadhi ya wasanii watakaokuwepo kwenye ziara hiyo wakiwe kwenye picha ya pamoja
Wengine ni Nay wa Mitego, Mwana FA, Khadija Kopa, Juma Nature, Warriors From the East, Madee, Young Killer, Jambo Squad, AY, Vanessa Mdee, Mashujaa Band, Rich Mavoko na Christian Bella.
No comments: