Kanye West ana furaha kubwa kuwa rafiki yake Jay-Z kesho Jumamosi atahudhuria harusi yake na Kim Kardashian.
Hata hivyo, bado Beyonce haijulikani kama atakuwepo. Kwa mujibu wa mtandao wa Celebrity Dirty Laundry, kwasababu ya drama iliyomhusisha yeye na mumewe pamoja na mdogo wake Solange Knowles, anaweza kuikosa lakini atabadili kama Rachel Roy akiwepo.

Rachel Roy
Rachel Roy ni mwanamke ambaye Solange anadaiwa kumfanya akwaruzane na Jay-Z kwenye MET Gala. Inadaiwa kuwa Rachel Roy alikuwa akijitongozesha kwa Jay-Z kwenye tukio hilo lililokuwa na watu wengi. Bahati mbaya, Solange alichukia na kumtuhumu shemeji yake anaweza kuwa anamsaliti dada yake na ndio maana alimpiga wakiwa kwenye lifti kama ilivyoonekana kwenye video iliyosambaa mtandaoni.Kama Rachel Roy atahudhuria harusi hiyo, ripoti zinadai kuwa Jay anaweza kumsaliti mkewe Bey na kuchepuka na Roy. Kama Beyonce akiona jina la Roy kwenye orodha ya wageni anaweza kubadili mawazo na kuhudhuria harusi hiyo ili kumlinda mumewe asiingiwe na majaribu ya urembo wa Rachel na kuvunja amri ya sita!!
Ripoti za Roy kujipendekezesha kwa Jay-Z hazijathibitishwa bado.
No comments: