Amesema mpaka kumaliza kurekodi wimbo huo walitumia siku nne ikiwa ni pamoja na siku moja ya kutengeneza beat na kutafuta melody.
Tudd amesema kwakuwa anafahamu ukubwa wa wasanii hao watatu, alijitahidi kufanya kazi ya uhakika kwakuwa itamtangaza kimataifa.
“Ni kitu ambacho nilikuwa nakitegemea kwamba huu wimbo utanifikisha mbali ndio maana wakati nafanya nilijitahidi na mimi mwenyewe kwamba ukisikiliza ni sound mpya ambayo watu wengi hawajawahi kuisikia,” amesema.
“Maana yangu ni kwamba mtu wa mbali anapoenda kuisikia aweze kuutambua muziki ambao upo hapa na sisi tuweze kusikika mbali zaidi kimasoko.”
No comments: