Jana Ijumaa (May 23) Kanye West na Kim Kardashian waliianza ratiba yao kuelekea siku ya harusi ya mwaka inayosubiriwa kwa hamu kubwa kwa kufanya ‘pre-wedding dinner party’ huko Paris, Ufaransa huku ndoa yenyewe ikitarajiwa kufungwa leo.
Kim na ndugu zake
Kwa mujibu wa ripoti, fataki zilitawala eneo la tukio, huku ikisemekana anga la eneo hilo siku ya jana lilikuwa ‘NO-FLY ZONE’, hakuna ndege yoyote iliyokatiza.
Maharusi wakiongea mbele ya wageni waalikwa
Jana mitaa ya Paris ilishuhudia pilikapilika za wageni na mapaparazi wakielekea eneo ilipofanyika sherehe ya chakula cha jioni kabla ya ndoa (pre-wedding dinner), iliyohudhuriwa na wageni wanaokadiriwa kufikia 100 wakiwemo dada zake Kim, Kourtney, Khloe, Kylie, Kendall na mama yake Kris Jenner na wageni wengine mbalimbali.
Usiku huo ulipambwa na burudani mbalimbali ikiwa ni pamoja na mwimbaji aitwaye Lana Del Rey.
.
Chupa 1,000 za champagne ziliandaliwa kwaajili ya wageni waalikwa waliohudhuria.
Chupa 1,000 za champagne ziliandaliwa kwaajili ya wageni waalikwa waliohudhuria.
Kwa mujibu wa Entertainment Tonight, maharusi watarajiwa Kimye waliwatangazia wageni waalikwa kuwa ndoa yao itafungwa siku inayofuata yaani leo Jumamosi (May 24) huko Italy.
Source: Daily Mail
No comments: