» » » Ubilionea wa Dr. Dre utaongeza maumivu kwa kampuni ya Monster kwa kosa walilofanya kummilikisha headphones zao

Kampuni ya Apple inaonekana kuwa imekubaliana na Dr Dre na mwenyekiti wa Interscope, Jimmy Lovine kununua headphones za Beats By Dre kwa $3.2 billion na kumfanya Dr Dre kuwa billionaire wa kwanza mwana hip hop.

Hata hivyo, undani wa deal hiyo inayomfanya Dr. Dre kuanza kushangilia mapema mgao mkubwa wa pesa hizo unageuka kuwa maumivu makubwa zaidi ya chumvi nyingi kwenye kidonda ambacho walikipata kampuni ya Monsters ambayo kiuhalisia ndiyo iliyoanzisha na kutengeneza headphones zilizobatizwa jina la Beats By Dre.



Kwa mujibu wa mtandao wa gizmodo, headphones ilianzishwa na Noel Lee mzaliwa wa Marekani mwenye asili ya China aliyekuwa anaishi San Francisco, ambaye alikuwa anafanya kazi ya kutengeneza cables na speaker tangu mwaka 1979 huku akijaribu kujitanua kwa kadri anavyoweza na kufanya ubunifu akiwa na kampuni yake ya ‘Monster’.

Noel Lee ambaye ni mlemavu wa miguu, alipata idea ya kutengeneza speaker lakini aligundua yuko nyuma ya wakati kwa kuwa muda huo tayari makampuni yalianza kuzalisha TV ambazo zina speaker ndani na hivyo hazikuhitaji speaker za nje kwa matumizi ya nyumbani.

Hata hivyo, Noel Lee alianza kufikiria kitu ambacho kingeweza kuwa rahisi kutumiwa na watu mbalimbali hata kama wanatembea kutoka sehemu moja kwenda nyingine na ndipo lilipozaliwa wazo la ‘headphones’.

Idea ya headphones ilivyoingia mikononi mwa Dre Dre na Jimmy Lovine kutoka kwa Monster:

Baada ya bwana Noel Lee kupata idea hiyo na kuifanyia utafiti na muundo mzima wa jinsi itakavokuwa, kabla hajaanza kufanya biashara hiyo alipata wazo kuwa ni vizuri wakimpata mtu maarufu ambaye atasaidia katika kuziuza headphones hizo.

Mtoto wa Noel Lee, Kelvin Lee amesimulia kuwa baba yake alimtuma Young Lee kwenda kuwatafuta watu wenye majina makubwa katika muziki na kujaribu kuongea nao.

“You gotta go get Usher, Mary J. Blige, U2.” Hayo yalikuwa sehemu ya maelekezo ya Noel Lee.

Akisimulia tukio hilo, Kelvin anasema kuwa wakati mwingine mambo inabidi yatokee hivyo tu, lakini mambo yangekuwa tofauti leo endapo aliyetumwa asingekutana na Jimmy Lovine wa Interscope. Huenda kusengekuwa na headphones za Beatz by Dre kama zilivyo sasa!

Ilikuwa kama Mungu amekutanisha idea ya Interscope na ya Monsters kwa kuwa wakati huo, Jimmy Lovine alikuwa inamtaka Dr Dre afanye endorsement kwenye raba (sneakers) ili wasitegemee tu kazi ya muziki kuingiza pesa, lakini Dr Dre alibadili mawazo yake, “f*ck sneakers, let’s make speakers.”

Idea ya kutengeneza speaker ilikubaliwa na Jimmy Lovine na kwa maelezo ya Jimmy Lovine na Dre hivyo ndivyo idea ya Beatz by Dre ilivyozaliwa.

Hata hivyo, familia ya Noel Lee inasema kuwa Dr Dre na Lovine hawaelezi ukweli wote kwa kuwa baada ya kukutana waliwashauri waachane na suala la kutengeneza speaker na kwa pamoja watengeneze headphones kwa kuwa wao walikuwa na teknolojia na akina Dr Dre walikuwa na uwezo wa kuuza zaidi. “Let’ build headphones together,” Noel Lee anakumbuka alivyowaambia na mshikamano huo ndio uliwavutia zaidi.

Hata hivyo, muda ulivyoenda Dr. Dre na Lovine walikuwa wanatafuta namna ya kumiliki idea yao wenyewe na hivyo kutangaza deal na kampuni nyingine ya ‘SLS’ lakini kwa bahati mbaya kwa kuchukua sample waliyoiona kwa Monsters, headphones zake hazikuwa na ubora wa hali ya juu kama za monsters.

Kelvin Lee anaeleza kuwa wakati huo hakuwa na uzoefu sana na biashara na alijikuta ametumia zaidi ya dola milioni moja za baba yake kwa ajili ya kutayarisha soko la headphones bila kumwambia baba yake kwa kuwa yeye aliamini baba yake alikuwa slow kuikamilisha deal hiyo.

Kwa kuwa tayari alikuwa ametumia pesa nyingi ya kampuni ya baba yake bila kumwambia, kutofanya biashara hiyo na Dre na Levine ikuwa hasara kubwa zaidi ambayo ingempa pressure baba yake hivyo Kelvin anasema ilimbidi awatafute Dr. Dre na Levine na kusaini nao mkataba huku mkataba ukiimiza kampuni yao, kwa muda huo aliwaza tu jinsi ya kurudisha hizo dola milioni kadhaa.

“It was beyond insubordination. I was going to lose the trust of my father. I already had millions of dollars of inventory. He would have killed me.” Amesema Kelvin Lee.

Kelvin ameeleza kuwa ilipofika wakati wa kusaini mkataba alijikuta akiwa amezungukwa na timu kubwa ya wanasheria na wafanyabiashara wakubwa hali iliyomchanganya kidogo kwa kuwa yeye alikuwa hana uzoefu katika ku-deal na biashara kubwa kiasi hicho peke yake.

Akiwa na nia ya kufanya juu chini arudishe fedha ya baba yake, matokeo yake alisaini mkataba ulioonesha kuwa kila kitu kinachohusiana na headphone hizo kitakuwa mali ya Jimmy na Dr Dre daima. Hii inamaanisha Noel na Kevin Lee waliwapa kila kitu Dre Dre na Jimmy Levine katika deal ya kwanza tu.

Hata hivyo, Beats Electronics wamekana kutumia teknolojia ya Monster na kueleza kuwa wana kila kitu chao ambacho kinawawezesha kuzalisha headphones na kwamba makampuni yote mawili ni marafiki.

“We have our own factories. We have control of everything. The sound...was always our thing—we have our own patented sound signature.” Wamesema Beats Electronics na kuongeza kuwa bado wanauhusiano mzuri tu na Monster.

Mtu wa ndani wa Monsters ametoa vielelezo vya documents ambazo zinaonesha michoro na maelezo ya Monster kuhusu headphones hizo yaliyokuwa yanatumwa kwa Beats Electronics.

Nae Noel Lee, amesisitiza kuwa Beats Electronics hawakuwa na mafundi (engineers), “

Absolutely not, they don't have any engineers. Beats had zero (engineering role).

Hata hivyo maelezo ya Monster kwa sasa ni kama hadithi tu ya ‘paukwa pakawa’ kwa kuwa hawana uwezo wowote wa kubadili wanachokiona.

Ningejua huja baada, hivi sasa Kelvin Lee anajiona mwenye makosa na analikumbuka kosa moja alilofanya lililogeuka kuwa faida kubwa leo kwa Dr Dre na Jimmy Levine ambao wanapewa $3.2 billion na Apple na benefits kibao.

Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply