Mirror amesema kuwa, kazi hii ipo katika hatua za mwisho za ukamilishwaji kabla ya kuachia hivi karibuni, ngoma ambayo inakwenda kwa jina Kokoro, ikiwa imefanywa na Nahreel, ikiwa imepangwa kuachiwa wiki ijayo.
Mirror pia ambaye amefanikiwa kufanya kolabo na msanii Jose Chameleone kutoka Uganda, amezungumza kuhusiana na kufanya kazi na staa huyu, na ujio wa kolabo hii ambayo amesema imewezekana kwa kazi kubwa aliyofanya msimamizi wa kazi zake Petit Man.
Mirror ameweka wazi kuwa, alikuwa na mpango wa kufanya remix ya kazi zake na Chameleone, lakini baada ya kukaa na kusikiliza baadhi ya kazi zake wakaamua kufanya kazi mpya kabisa, kazi ambayo itatoka baada ya Kokoro kutoka.
No comments: