Brazia ni kitu nyeti sana lakini wadada wengi wanashindwa kulichukulia kwa uzito wake.
Kati ya vitu ambavyo wanawake wengi hukosea ni kutokujua size ya maziwa yao na ni brazia ya aina gani inawafaa.
Kati ya vitu ambavyo wanawake wengi hukosea ni kutokujua size ya maziwa yao na ni brazia ya aina gani inawafaa.
Unakuta mwanadada amevalia nguo yake nzuri lakini ukimwangalia kifuani amegawanyisha maziwa yake katika sehemu mbili. Hii yote inatokana na kutokujua ni aina gani ama ni saizi gani ya brazia ambayo anatakiwa kuivaa.
AINA ZA BRAZIA.
Kuna aina mbalimbali za brazia
Kuna aina mbalimbali za brazia
- Kuna zenye sponge hizi hupendelewa sana na watu wenye maziwa madogo..lakini si kwamba wenye maziwa makubwa hawaruhusiwi la hasha! Bali kwanza jijue unavaa saizi gani ndipo ununue hiyo brazia
- Kuna zenye chuma. Hizi husaidia sana kuweka maziwa sawa. Wanawake wengi wanziogopa wakihofia zitawaumiza lakini kwa uhalisia si kweli. Jambo unalotakiwa kuangalia kabla ya kununua hizi zenye chuma ni kuangalia ambazo ni imara na chuma yake iwe kwa ndani na haina dalili yoyote ya kutokeza kwa nje.
- Kuna zenye mikanda minene na zenye mikanda myembamba. Mikanda midogo inasaidia sana wale wenye maziwa makubwa kwani maziwa yanapokuwa makubwa huwa mazito. Kwa hiyo mikanda mipana husaidia kukupa muonekano mzuri kifuani. Na wale wenye maziwa madogo mikanda myembamba huwafaa Zaidi wenye maziwa madogo.
- Kuna ambazo hazina mikanda kabisa. Hizi hufaa sana pale unapoamua kuvaa nguo za wazi ama nguo ambazo zinaishia kifuani. Jithidi upate saizi inayofunika ziwa kabisa.
- Kuna zenye mikanda ya plastiki(wengine huita mikanda ya maji) hii pia husaidia sana pale unapovalia nguo yenye mikanda midogo. Hii itakupa mwonekano mzuri kwani maziwa yako yatakaa vizuri na hakutokuwa na rangi ya brazia itakayoonekana huku na huko kwenye kivazi chako ulichovaa.
RANGI YA BRAZIA NA RANGI YA NGUO.
Pale unapovaa nguo nyeupe, iwe blauzi ama gauni unashauriwa kuvalia brazia nyeusi ili kupata muonekano maridhawa. Rangi mbalimbali zinapendeza kwa nguo ambazo hazioneshi yani nzito. Vilevile pale unapopendelea mikanda myembamba ya brazia ionekane kwa nje, hakikisha mikanda inaendana na moja ya rangi ya nguo uliyovaa ama moja ya vitu ulivyoambatana navyo kama vile viatu, mkoba mkanda au hata kibanio cha nywele.

JE NI AFYA KULALA NA BRAZIA?
Si sahihi kulala ukiwa umevaa brazia, baada ya kubana maziwa mda wote wa mchana ni vyema wakati wa usiku ukaitoa ili kuyapa nafasi ya kupumua na vilevile kuruhusu misuli kupumzika. Hii itasaidia damu kuzunguka vizuri.

No comments: