Habari kwa Ufupi :

    3:00 PM
» » » Don Jazzy Amuajiri Mfanyakazi Wa Airport Aliyefukuzwa Baada Ya Kumpa Msaada

C.E.O wa label ya Mavin Don Jazzy amempa ajira mfanyakazi wa Delta Airline ambaye amefukuzwa kazi baada ya kumruhusu Don Jazzy kuendesha gari ndogo ambalo hutumika kubebea mizigo ndani ya airport (airport cart) akiwa kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa Murtala Mohammed , Lagos,Nigeria.


Mfanyakazi huyo ambaye hajajulikana jina lake amefukuzwa kwa kosa la kumruhusu don Jazzy kuendesha kigari hicho ndani ya uwanja wa ndege wakati akijua ni kinyume na sheria za ndege hiyo.

Don Jazzy alirekodi video akiendesha kigari hicho wakati akiwa kwenye uwanja huo ndege akisafiri kwenda South Africa kwenye MTV music awards huku mfanyakazi huyo akiwa amekaa pembeni.



Taarifa za kufukuzwa kazi kwa mfanyakazi huyo kilimshtua producer huyo ambaye ameamua kuokoa jahazi kwa kumpa ajira nyingine katika label yake ambayo yenye wasanii kwakubwa kama Tiwa Savage, Dr Sid na D’Banj.

Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Picha: Pitbull na Jennifer Lopez wapamba sherehe za ufunguzi wa kombe la dunia 2014, Brazil
»
Previous
Music: Maua Sama – Let Them Know

No comments:

Leave a Reply