Baada ya kukata ngembe za waingereza usiku wa kuamki hii leo huko nchini Barzil, FC Barcelona wametangaza kumuwekea dau la paund million 52 shujaa wa kikosi cha timu ya taifa Uruguay Luis Alberto Suarez Diaz.
FC Barcelona wameonyesha jeuri hiyo ya fedha kutokana na hitaji la mshambuliaji linalowakabili kwa sasa, ambapo imeaminika huenda Luis Suarez, akatosha katika kufikia malengo waliyojiwekea chini ya meneja mpya Luis Enrique.
Klabu hiyo nguli barani Ulaya, imesssitiza kuwa tayari kutoa kiasi hicho cha pesa sambamba na kukubali kumuachia mshambulia wao kutoka nchini Chile, Alexis Sanchez ambae hayupo kwenye mipango ya meneja huyo aliyerithi mikoba kutoka kwa meneja wa nchini Argentina Gerardo Daniel "Tata" Martino.
Hata hivyo pamoja na mbwembwe zote hizo za FC Barceklona, uongozi wa klabu ya Liverpool haujazungumza lolote katika kipindi hiki ambacho tetesi za usajili huchukua nafasi kubwa katika vyombo vya habari.
Inahofiwa huenda Liverpool wakaendeleza msimamo wao wa kutokumuachia mshambuliaji huyo kama walivyofanya mwanzoni mwa msimu uliopita, ambapo Luis Suarez alitakiwa na klabu ya Arsenal kwa ada ya uhamisho wa paund million 40.

No comments: